Jeromu Emiliani (Venisi, Italia, 1486Somasca, karibu na Bergamo, 8 Februari 1537) alikuwa padri na mtawa nchini Italia.

Mt. Jeromu Emiliani.
Mt. Jeromu Emiliani.

Papa Klementi XIII alimtangaza mtakatifu mwaka 1767, halafu Papa Pius XI alimtangaza msimamizi wa mayatima mwaka 1928.

Sikukuu yake ni tarehe 8 Februari[1].

Maisha hariri

Kwanza alikuwa askari, akitumia ujana wake katika anasa na ukatili, lakini baada ya kutupwa gerezani na maadui wake, alimuongokea Mungu akaacha kazi hiyo akawapa fukara mali yake yote ili ajitoe mhanga pamoja na wenzake kadhaa kuwahudumia maskini, hasa mayatima na wagonjwa.

Baada ya kupata upadri (1518) alianzisha hivyo Utawa wa Makleri walioitwa Wasomaska.

Wakati wa kuhudumia wenye tauni, aliambukizwa nao akafariki kwa ugonjwa huo wa kutisha.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  • "Sala ya Kanisa - Vipindi vya Liturjia", Toleo la Tatu 1996, Ndanda - Peramiho: Benedictine Publications, uk.1283

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.