Karamba Diaby (amezaliwa 27 Novemba 1961 [2]) ni mwanakemia Mjerumani mzaliwa wa Senegal na mwanasiasa wa chama cha SPD aliyechaguliwa mbunge wa Bunge la Shirikisho (Bundestag) tangu mwaka 2013.

Karamba Diaby


Mbunge wa kitafa Ujerumani (Bundestag)

tarehe ya kuzaliwa 27 Novemba 1961 (1961-11-27) (umri 63)
Marsassoum, Senegal
chama Bendera ya Ujerumani Ujerumani:
Chama cha Kijamaa-Kidemokrasia cha Ujerumani (SPD)
Bendera ya Umoja wa Ulaya Umoja wa Ulaya:
Party of European Socialists
watoto 3
makazi Halle (Saale, Ujerumani
mhitimu wa Chuo Kikuu cha Cheikh Anta Diop
Chuo Kikuu cha Martin Luther cha Halle-Wittenberg[1]

Maisha ya awali na elimu

hariri

Diaby alikulia huko Marsassoum nchini Senegal. Alikuwa mtoto mdogo kati ya wanne; alilelewa na dada yake baada ya kuwa yatima akiwa na umri wa miaka 7. [3] Baada ya kuhitimu kwenye Chuo Kikuu cha Cheikh Anta Diop, aliondoka Senegal kusoma kemia huko Ujerumani Mashariki alipopokea diploma yake 1991. Alibaki Ujerumani katika kipindi cha maungano wa Ujerumani ya Mashariki na Magharibi wa mwaka 1991. Mnamo 1996 alipata pata shahada ya uzamivu [1]. Baadaye alianza kujihusisha na harakati za kisiasa na kijamii na kwenye mwaka 2009 alijiunga na Chama cha Kijamaa-Kidemokrasia cha Ujerumani (SPD). Mwaka uleule alichaguliwa kama diwani katika halmashauri ya mji wa Halle (Saale), Saxonia-Anhalt.

Mnamo Septemba 22, 2013, Diaby alichaguliwa kuwa mbunge wa kitaifa kupitia orodha ya kijimbo ya SPD katika Saksonia-Anhalt.

Diaby alikuwa mmoja wa wabunge wawili wenye asili ya Kiafrika katika bunge Ujerumani, pamoja na Charles M. Huber (aliyezaliwa na baba wa Senegal na mama wa Ujerumani), mbunge wa Chama cha CDU. [4]

Diaby alirudishwa bungeni mwaka 2017 kupitia orodha ya kijimbo ya SPD. Alikuwa naibu mwenyekiti wa Kamati ya Haki za Binadamu na Misaada ya Kihisani na kama mjumbe kamili wa Kamati ya Elimu, Utafiti na Tathmini ya Teknolojia. [5]

Mbali na majukumu yake ya kikamati, Diaby ni naibu mwenyekiti wa Kikundi cha Mahusiano ya Kirafiki na bunge za Nchi za Lugha ya Kifaransa za Afrika Magharibi na Kati ( Guinea ya Ikweta, Benin, Burkina Faso, Côte d'Ivoire, Gabon, Guinea, Kamerun, Jamhuri ya Kongo, Mali, Niger, Senegal, Togo, Chad, Jamhuri ya Afrika ya Kati ). Tangu 2019, amekuwa mwanachama wa ujumbe wa Ujerumani kwa Mkutano wa Wabunge wa Ufaransa na Ujerumani. Yeye pia ni sehemu ya Mtandao wa Wabunge wa Elie Wiesel wa Kuzuia Mauaji ya Kimbari na Kikatili na dhidi ya Kukanushwa kwa Mauaji ya Kimbari. [6] Mnamo mwaka wa 2020, alianzisha kikundi cha wabunge wa vyama tofauti kinachofanya kazi juu ya kukubali watu walio tofauti na wengi katika jamii (diversity) na kupinga ubaguzi wa rangi. [7]

Ofisi ya Diaby mjini Halle ilipigwa risasi mnamo 15 Januari 2020. [8]

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2021 alirudishwa bungeni, akishinda mara ya kwanza moja kwa moja jimbo la uchaguzi wa Halle baada ya kupata asilimia 28.8[9] [10]

Maisha binafsi

hariri

Diabi alioa mke Mjerumani Ute na kuzaa naye watoto watatu. Anapenda kulima bustani yake, baada ya kuandika tasnia yake ya PhD kuhusu kemia kwenye bustani za mjini na kujiunga na shirika la wanabustani wadogo huko Halle.

Marejeo

hariri

Tovuti za Nje

hariri

Dr. Diaby kwenye tovuti ya Facebook Tovuti rasmi ya Dr Diaby (Kiingereza)