Wakaramojong

(Elekezwa kutoka Karimojong)

Wakaramojong au Wakarimojong ni kabila la watu wanaojihusisha na kilimo na ufugaji hasa wanaoishi kaskazini-mashariki mwa Uganda.

Lugha yao inajulikana kama Kikaramojong au Kikarimojong, na ni sehemu ya kundi la lugha za Kinilo-Sahara.

Historia hariri

Wakaramojong wanaishi katika kusini mwa mkoa wa Karamoja, kaskazini-mashariki mwa Uganda, ambao ni asilimia kumi ya nchi ya Uganda. Kulingana na wanaanthropolojia WaKaramojong ni sehemu ya kundi lililohamia kutoka Ethiopia katika miaka ya 1600 BK na kugawanywa katika matawi mawili, huku tawi moja likihamia nchi ya Kenya na kuunda kundi la Wakalenjin na nguzo ya Wamasai. Tawi lingine lililojulikana kama Waateker lilihamia upande wa magharibi.

Waateker waligawanyika zaidi katika makundi kadhaa, wakiwa ni pamoja na Waturkana katika nchi ya Kenya, Wateso, Wadodoth au Wadodos, Wajie, Wakaramojong na Wakumam nchini Uganda, pia Wajiye na Watoposa kusini mwa Sudan: wote hawa wakijulikana kama "Kundi la Kiteso" au "Kundi la Karamojong".

Wakaramojong walikuwa wanajulikana awali kama Wajie. Jina Karamojong lilitokana na kauli "Ekar ngimojong", linamaanisha "watu wakongwe hawaweza kutembea zaidi". Kulingana na utamaduni, kundi la watu hawa, ambao sasa wanajulikana kama Wakaramojong, wanasemekana kuhamia kutoka Ethiopia kati ya miaka ya 1600 na 1700 BK kama kundi moja linalojulikana kama Wajie. Walipofika mpakani mwa Kenya na Ethiopia, inasemekana kuwa waligawanyika katika makundi kadhaa: Waturkana, Watoposa, na Wadodoth. Kati ya makundi haya tatu, Waturkana waliamua kubaki waliko sasa. Kundi la pili ambalo baadaye lilikuja kujulikana kama Watoposa liliendelea moja kwa moja hadi Sudan. Kundi la tatu, Wadodoth waliamua kubaki katika sehemu ya Apule katika sehemu ya kaskazini ya Karamoja. Kundi kuu liliendelea upande wa kusini na baada ya kufika katika wilaya kuu ambayo sasa ni ya Jie, makundi haya makuu yanaripotiwa kugawanyika katika makundi matatu zaidi na kuhamia kusini zaidi: Wapia, Wabokora, na Wamatheniko. Kundi la tatu la Wamatheniko, lilienda upande wa magharibi na kuunda lugha za Kiteso, Kikumam na Kilangi. Lilikuwa kundi hilo la mwisho ambalo lilisafiri zaidi ambalo linasemekana kutumia kauli ya "watu wakongwe hawaweza kutembea zaidi".

Lugha hariri

Katika lugha ya Kikaramojong, watu wa lugha hii hutumia viambishi awali ŋi- na na- mtawalia, ukosefu wa kiambishi awali huonyesha nchi au sehemu wanamoishi. Matawi yaliyotajwa hapo awali kutoka lugha zinazozungumza Kiateker yanaweza kuelewana kwa kiasi kikubwa au kidogo. Lugha ya Kilango nchini Uganda pia ina uhusiano wa kiasi fulani na lugha ya ŋiKarimojong, na hii inathibitishwa na majina yanayofanana miongoni mwa mambo mengine, ingawa wana njia fulani ya kuzungumza ambayo walikopa kutoka lugha ya Kiluo.

Utamaduni hariri

Shughuli kuu ya maisha ya Wakaramojong ni ufugaji, ambao una umuhimu wa kijamii na kitamaduni. Kulima mazao ni shughuli ya pili na huratibiwa tu katika maeneo ambayo yanaweza kulimwa.

Kutokana na hali ya hewa ya jangwa katika eneo hilo, Wakaramojong walikuwa daima wanajaribu njia tofauti za ufugaji kama vile kuwahamisha wanyama katika maeneo tofauti ambazo zina nyasi kwa ajili ya malisho, ambapo kwa muda wa miezi 3-4 kwa mwaka, wao walihamisha mifugo yao katika wilaya jirani kutafuta maji na malisho ya wanyama wao.

Upatikanaji wa chakula na maji daima ni wa wasiwasi na ina athari kwenye mwingiliano wa kundi la Wakaramojong na makundi mengine ya kikabila.

Migogoro hariri

Wakaramojong wamekuwa wakihusika katika migogoro mbalimbali unaozingatia mazoezi ya wizi wa wanyama.

Wakaramojong daima wanahusika katika vita na majirani wao nchini Uganda, Sudan na Kenya kutokana na wizi wa mifugo wa mara kwa mara. Hii inaweza kutokana na imani za mila kuwa Wakaramojong wanamiliki wanyama wote kwa haki ya Mungu, lakini pia kwa sababu mifugo, hasa ng'ombe, ni muhimu katika mazungumzo ya kutoa mahari kwa ajili ya bibiarusi. Wanaume hutumia wizi wa mifugo kama haki ya kifungu na njia ya kuongeza mifugo yao ili kupata heshima.

Katika miaka ya hivi karibuni maumbile na matokeo ya wizi wa mifugo yameongezeka na kuwa hatari kwani kabila ya Wakaramojong limekuwa likinunua bunduki aina ya AK47 kwa ajili ya migogoro hiyo. [Serikali]] ya Uganda imejaribu kuingilia biashara hiyo.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wakaramojong kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.