Karoli Borromeo
Karoli Borromeo (2 Oktoba 1538 – 3 Novemba 1584) alikuwa kardinali na askofu mkuu wa Milano nchini Italia.
Aliongoza jimbo hilo kubwa kama mchungaji halisi tena makini kwa mahitaji wa Kanisa la wakati wake: aliitisha na kuongoza sinodi mbalimbali, alianzisha seminari kwa ajili ya malezi ya waklero, alitembelea mara kadhaa kundi lake lote ili kustawisha maisha ya Kikristo akatoa sheria nyingi ili kuokoa milele watu [1].
Ametambuliwa na Kanisa Katoliki kuwa mtakatifu.
Maisha
haririKaroli Borromeo alizaliwa katika mji wa Arona katika mkoa wa Lombardia nchini Italia mwaka 1538.
Baada ya kupata shahada ya tatu katika sheria za serikali na za Kanisa, alifanywa kardinali na mjomba wake, Papa Pius IV, akachaguliwa kuwa askofu mkuu wa Milano.
Hata hivyo aliishi maisha magumu ya kifukara, hata alifananishwa kwa mbwa katika nyumba ya bwana wake.
Alikuwa mchungaji bora wa kundi lake. Mara kwa mara alipitia parokia zote jimboni mwake, aliitisha mikutano, hasa sinodi 11, aliweka sheria za kufaa kwa watu, na alijitahidi kuhimiza maadili ya Kikristo.
Alitoa huduma nyingi kwa maskini, kama vile shule za bure, mabweni, nyumba za wasichana ili kuwatoa katika ukahaba, n.k.
Ndiye aliyefanikisha zaidi sehemu ya mwisho wa Mtaguso wa Trento na utekelezaji wake, kama vile uanzishaji wa seminari kwa ajili ya malezi ya mapadri wapya.
Alianzisha pia shirika la Oratorio jimboni mwake.
Tazama pia
haririTanbihi
haririMarejeo
hariri- "Sala ya Kanisa - Vipindi vya Liturjia", Toleo la Tatu 1996, Ndanda - Peramiho: Benedictine Publications, uk.1562
- A. Sala, Documenti circa la vita e la gesta di Borromeo (4 vols., Milan: 1857–1859)
- Chanoine Silvain, Histoire de St Charles Borromeo (Milan: 1884)
- A. Cantono, "Un grande riformatore del secolo XVI" (Florence: 1904); "Borromus" in Herzog-Hauck, Realencyklopädie (Leipzig: 1897).
Viungo vya nje
hariri- The Life of St. Charles Borromeo, Confessor and Archbishop of Milan Ilihifadhiwa 5 Machi 2016 kwenye Wayback Machine.
- University of San Carlos, Cebu City, Philippines Official Site Ilihifadhiwa 29 Novemba 2020 kwenye Wayback Machine.
- Saint Charles Borromeo Seminary, Archdiocese of Philadelphia
- Pietro Canetta, "Biography of Carlo Borromeo" (in Italian), Magazzeno Storico Verbanese
- "St. Charles Borromeo", Catholic Encyclopedia
- "St. Charles Borromeo, Cardinal, Archbishop of Milan, Confessor", Butler's Lives of the Saints
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |