Kaunti ya Kirinyaga

Kaunti ya Kirinyaga ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Kaunti ya Kirinyaga
Kaunti
Vijana wakilima katika mradi wa umwagiliaji wa Mwea
Nembo ya Serikali
Kirinyaga County in Kenya.svg
Kaunti ya Kirinyaga katika Kenya
Nchi Kenya
Namba20
IlianzishwaTarehe 4 Machi, 2013
Ilitanguliwa naMkoa wa Kati
Makao MakuuKutus(Rasmi)
Miji mingineKerugoya, Sagana, Wang'uru
GavanaAnne Mumbi Waiguru
Naibu wa GavanaPeter Njagi Ndambiri
SenetaDaniel Karaba Dickson
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa)Purity Wangui Ngirici
Bunge la KauntiBunge la Kaunti ya Kirinyaga
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa20
Maeneo bunge/Kaunti ndogo4
Eneokm2 1 478.3 (sq mi 570.8)
Idadi ya watu610,411
Wiani wa idadi ya watu413
Kanda mudaSaa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovuti kirinyaga.go.ke

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 610,411 katika eneo la km2 1,478.3, msongamano ukiwa hivyo wa watu 413 kwa kilometa mraba[1].

Makao makuu yako Kerugoya/Kutus.

Jiografia

hariri

Kaunti ya Kirinyaga imepakana na Nyeri (magharibi), Murang'a (kusini magharibi) na Embu (mashariki).

Mlima kenya na msitu unaouzunguka uko kaskazini mwa kaunti. Theluji ambayo huyeyuka kutoka Mlima Kenya hutengeneza mito, k.v. Mto Thiba na Mto Kiganjo. Mito mingine iliyo katika kaunti hii ni Mto Sagana, Mto Nyamindi, Mto Rupingazi, Mto Thiba, Mto Rwamuthambi and Mto Ragati[2].

Kirinyaga huwa na tabianchi tropiki na hupata misimu miwili ya mvua.

Utawala

hariri

Kaunti ya Kirinyaga imegawanywa katika maeneo bunge yafuatayo[3]:

Eneo Bunge Kata
Mwea Mutithi, Kangai, Wamumu, Nyangati, Murindiko, Gathigiriri, Teberer
Gichugu Kabare, Baragwi, Njukiini, Ngariama, Karumandi
Ndia Mukure, Kiine, Kariti
Kirinyaga Central Mutira, Kanyekini, Kerugoya, Inoi

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [4]

hariri
  • Kirinyaga Central 122,740
  • Kirinyaga East 135,559
  • Kirinyaga West 114,660
  • Mwea East 132,554
  • Mwea West 104,828
    • Mt. Kenya Forest 70

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
  2. "Kirinyaga County Government". Iliwekwa mnamo 2018-04-30. {{cite web}}: Text "About Us" ignored (help)
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-09-04. Iliwekwa mnamo 2021-09-04.
  4. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.