Kaunti ya Tharaka-Nithi

Kaunti ya Tharaka-Nithi ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Kaunti ya Tharaka-Nithi
Kaunti
Nembo ya Serikali
Tharaka-Nithi County in Kenya.svg
Kaunti ya Tharaka-Nithi katika Kenya
Coordinates: 0°18′S 38°0′E / 0.300°S 38.000°E / -0.300; 38.000
Nchi Kenya
Namba13
IlianzishwaTarehe 4 Machi, 2013
Ilitanguliwa naMkoa wa Mashariki
Makao MakuuKathwana
Kikao cha SerikaliChuka
GavanaMuthomi Njuki
Naibu wa GavanaFrancis Nyamu Kagwima
SenetaKithure Kindiki
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa)Beatrice Nkatha Nyaga
Bunge la KauntiBunge la Kaunti ya Tharaka Nithi
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa15
Maeneo bunge/Kaunti ndogo3
Eneokm2 2 564.4 (sq mi 990.1)
Idadi ya watu393,177
Wiani wa idadi ya watu153
Kanda mudaSaa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovutitharakanithi.go.ke

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 393,177 katika eneo la km2 2,564.4, msongamano ukiwa hivyo wa watu 153 kwa kilometa mraba[1]..

Serikali huketi Chuka, ingawa makao makuu rasmi ni Kathwana.

Jiografia hariri

Kaunti ya Tharaka Nithi imepakana na kaunti za Meru, Embu, Kirinyaga, Nyeri na Kitui.

Ina sehemu ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kenya upande wa magharibi.

Mto Tana hupitia katika kaunti hii. Mito inayotiririsha maji ndani ya Mto Tana na hupitia Tharaka Nithi kutoka Mlima Kenya ni: Mto Mutonga, Mto Thingithu, Mto Kathita, Mto Thanantu, Mto Thangatha, Mto Kithinu na Mto Ura[2].

Utawala hariri

Kaunti ya Tharaka Nithi imegawiwa katika maeneo bunge yafuatayo:

Eneo bunge Kata
Maara Mitheru, Muthambi, Mwimbi, Ganga, Chogoria
Chuka/Igambango'mbe Mariani, Karingani, Magumoni, Mugwe, Igambang’ombe
Tharaka Gatunga, Mukothima, Nkondi, Chiakariga, Marimanti

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [3] hariri

  • Igambang'ombe 53,210
  • Maara 114,894
  • Meru South 91,080
  • Tharaka North 58,345
  • Tharaka South 75,250
    • Mt. Kenya Forest 398

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
  2. "About - County Government of Tharaka Nithi". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-12-04. Iliwekwa mnamo 2018-04-15.
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.

Viungo vya nje hariri