Kaunti ya Embu
Kaunti ya Embu ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.
Kaunti ya Embu | |||
---|---|---|---|
Kaunti | |||
Sanamu iliyo kati mwa mji wa Embu | |||
| |||
Land of opportunities | |||
Embu County in Kenya.svg Kaunti ya Embu katika Kenya | |||
Nchi | Kenya | ||
Namba | 14 | ||
Ilianzishwa | Tarehe 4 Machi, 2013 | ||
Ilitanguliwa na | Wilaya ya Embu (Kenya) | ||
Makao Makuu | Embu | ||
Miji mingine | Siakago, Kírítirí, Manyatta, Runyenjes | ||
Gavana | Cecily Mbarire | ||
Naibu wa Gavana | Kínyua Múgo | ||
Seneta | Múndigi Túonaga | ||
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa) | Pamela Njoki | ||
Bunge la Kaunti | Bunge la Kaunti ya Embu | ||
Spika | Thirikú | ||
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa | 20 | ||
Mahakama | Mahakama Kuu, Embu | ||
Maeneo bunge/Kaunti ndogo | 4 | ||
Eneo | km2 2 820.7 (sq mi 1 089.1) | ||
Idadi ya watu | 608,599 | ||
Wiani wa idadi ya watu | 216 | ||
Kanda muda | Saa za Afrika Mashariki (UTC+3) | ||
Tovuti | embu.go.ke |
Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 608,599 katika eneo la km2 2,820.7, msongamano ukiwa hivyo wa watu 216 kwa kilometa mraba[1].
Makao makuu Embu Town (Kírímarí)
Jiografia
haririKaunti ya Embu inapakana na kaunti za Tharaka Nithi (kaskazini), Machakos (kusini), Kitui (mashariki) na Kirinyaga (magharibi). Sehemu ya Mbeere hujumlisha 74% ya kaunti na ni kavu kuliko sehemu zingine. Sehemu nyingi za kaunti hupata mvua ya kiwango cha mm 500[2].
Mto Tana hupitia katika kaunti hii, upande wa kusini na mashariki katika mpaka na kaunti za Machakos na Kitui. Sehemu hii ya Mto Tana huwa na malambo ya uzalishaji umememaji, yanayojulikana kama Seven Forks Dams.
Mbuga zilizo katika kaunti hiii ni sehemu ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kenya na Hifadhi ya Kitaifa ya Mwea inayopakana na Bwawa la Kamburu.
Utawala
haririKaunti ya Embu imegawanywa katika maeneo bunge yafuatayo[3]:
- Embu East 129,564
- Embu North 79,556
- Embu West 127,100
- Mbeere South 163,476
- Mbeere North 108,881
- Mt. Kenya Forest 22
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
- ↑ Fausta Mbura Njiru. "Hydrological information for dam site selection by integrating geographic information system GIS and analytical hierarchical process AHP" (PDF). Iliwekwa mnamo 2018-04-16.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-09-04. Iliwekwa mnamo 2021-09-04.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kaunti ya Embu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |