Kiolwa cha angani
Kiolwa cha angani (pia: gimba la angani, kwa Kiingereza: astronomical object au celestial body) ni jina la jumla kwa ajili ya vitu vinayopatikana katika anga ya ulimwengu.
| |||||||
Mifano ya violwa vya angani |
Kwa Kiingereza istilahi "object" (kiolwa) na "body" (gimba) mara nyingi hutumiwa kama visawe. Lakini ilhali kila gimba la anga-nje ni pia kiolwa cha anga-nje, kinyume chake si kweli. Gimba la anga-nje ni kitu kimoja cha pekee, kama vile sayari, mwezi, asteroidi. Kiolwa cha anga-nje ni wazo pana zaidi, likitaja pia mambo kama galaksi au nebula yenye sehemu nyingi ndani yake.
Kati ya violwa vya anga-nje huhesabiwa:
- Jua
- Sayari
- Sayari kibete
- Miezi
- Vimondo (pia meteori au meteroidi)
- Asteroidi
- Nyotamkia
- Nyota
- Galaksi
- Nebula
- Mawingu katika anga
Hivyo vyote ni violwa asilia. Vitu vilivyoko kwenye anga-nje vilivyotengenezwa na binadamu ni vyombo vya anga-nje. Hapa kuna swali kama mabaki kutokana na vyombo vya anga-nje vilivyovunjika au takataka ya angani yanayotokana na safari za anga-nje yanastahili kuitwa kwa neno hili.
Elimu ya violwa vya anga-nje ni astronomia.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kiolwa cha angani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |