Macau

(Elekezwa kutoka Makau)

Macau (tamka: Makau; kwa Kichina: 澳門; pinyin: Àomén; Jyutping: Ou3 Mun4) ni eneo dogo la Jamhuri ya Watu wa China lenye utawala wa pekee kwenye pwani ya Bahari ya Kusini ya China.

澳門特別行政區
Região Administrativa Especial de Macau
Mkoa wenye utawala wa pekee wa Jamhuri ya Watu wa China
Bendera ya Macau Nembo ya Macau
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: --
Wimbo wa taifa: (kama China)
Lokeshen ya Macau
Mji mkuu -- 1
22°10′ N 113°33′ E
' (mji ulikuwa na tarafa ndani yake zilizofutwa tangu 2000)
Lugha rasmi · Kichina
· Kireno
Serikali
Mtendaji mkuu

Ho Iat Seng
Kuanzishwa kwa mji
Iliundwa na wenyeji Wachina
kutwaliwa na Ureno
koloni ya Ureno
Mkoa wa pekee wa China


Tangu karne ya 5 BK
1557
31 Agosti 1862
20 Desemba 1999
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
30.3 km² (--)
0
Idadi ya watu
 - 2015 kadirio
 - 2011 sensa
 - Msongamano wa watu
 
642,900 (ya 167)
552,503
18,568/km² (ya 1)
Fedha Pataca ya Macau (MOP)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
MST (UTC+8)
--
Intaneti TLD .mo
Kodi ya simu +853

-

1 Mji mkuu ulikuwa "Cidade do Nome de Deus de Macau" au rasi ya Macau yenyewe; makao makuu ya serikali ya koloni yalikaa kwenye tarafa ya Sao Lorenco.
2 Habari kutoka Direcção dos Serviços de Estatística e Censos (ofisi ya takwimu ya Macau )


Makao Makuu ya serikali ya Macau

Hali halisi eneo ni rasi ya Macau pamoja na visiwa viwili vidogo, jumla ni km² 32.9 na kuna wakazi 667,400 (mwishoni mwa mwaka 2018). Msongamano wa Macau wenye watu 21,340 kwa kilomita ya mraba ndio msongamano mkubwa kabisa duniani kote.

Tarehe 23 Oktoba 2018 rais wa China Xi Jinping alizindua rasmi daraja la baharini refu kuliko yote duniani (kilometa 55) linalounganisha Hong Kong, Macau na China bara (mji wa Zhuhai).

Koloni la Ureno

hariri

Macau ilikuwa kituo cha Ureno tangu karne ya 16 na Wareno wakaikodi tangu mwaka 1670.

Macau kama koloni ilithibitishwa katika Mkataba wa Beijing wa mwaka 1887 kati ya China na Ureno.

Macau kama eneo la pekee la China

hariri

Mwaka 1999 ilirudishwa mikononi mwa serikali ya China lakini kwa hali ya pekee inayofanana na ile ya eneo la jirani la Hong Kong.

Hivyo Macau inaendendelea kuratibu yenyewe mambo yake kwa ndani, lakini madaraka kuhusu usalama, jeshi na siasa ya nje yako Beijing.

Wakazi wengi (88.4%) ni Wachina asilia, 1.8% ni Wareno. Kwa kuwa uzazi ni mdogo sana, kuna wahamiaji wengi, hasa Wafilipino (4.6%) na Wavietnam (2.4%).

Lugha rasmi ni Kichina na Kireno. Katika matumizi ya kawaida, Kichina cha Canton kinaongoza (87.5%), na Kiingereza kina waongeaji wengi (2.8%) kuliko Kireno (0.7%).

Upande wa dini, 58.9% wanafuata dini za jadi za Kichina (mchanganyiko wa Ukonfusio na Utao), 17.3% ni Wabuddha au Watao, 7.2% ni Wakristo. 15.4% hawana dini yoyote.

Uchumi

hariri

Uchumi wa Macau hutegemea utalii na hasa michezo ya kamari. Kuna pia viwanda vya nguo.

Tazama pia

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Taarifa za jumla
Utalii
Malezi
Michezo

22°10′N 113°33′E / 22.167°N 113.550°E / 22.167; 113.550

Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


  Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Macau kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.