Kisomali

(Elekezwa kutoka Kisomalia)

Kisomali (kwa mwandiko wa Kilatini: Af-Soomaali; Osmanya: 𐒖𐒍 𐒈𐒝𐒑𐒛𐒐𐒘 [æ̀f sɔ̀ːmɑ́ːlì]) ni lugha ya Kiafrika-Kiasia nchini Somalia, Ethiopia, Kenya na Jibuti inayozungumzwa na Wasomali.

Kupitia kwa Wasomali wahamiaji, Kisomali huzungumzwa katika nchi nyingine nyingi kama vile Kanada, nchi mbalimbali za Ulaya na za Uarabuni.

Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kisomali nchini Somalia ilihesabiwa kuwa watu 8,340,000. Pia kuna wasemaji 4,610,000 nchini Ethiopia (2007), 2,386,222 nchini Kenya (2009), na 297,200 nchini Jibuti (2006).

Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kisomali kiko katika kundi la lugha za Kikushi.

Lugha ya Kisomali imeandikwa rasmi kwa alfabeti ya Kilatini ingawa alfabeti ya Kiarabu na maandishi kadhaa ya Kisomali kama vile Osmanya, Kaddare na maandishi ya Borama yanatumiwa kwa njia isiyo rasmi.

Uenezi wa Kisomali

hariri

Lugha ya Kisomali inazungumzwa katika maeneo yanayokaliwa na Wasomali ya Somalia, Jibuti, Ethiopia, Kenya, Yemeni na diaspora ya Somalia.

Kisomali ndiyo lugha inayozungumzwa zaidi ya Kikushi katika eneo hilo ikifuatiwa na Kioromo na Kiafari.[1]

Mnamo mwaka 2019, kulikuwa na takriban wazungumzaji milioni 21.8 wa Kisomali, walioenea katika Somalia Kuu (Greater Somalia) ambapo karibu milioni 7.8 waliishi Somalia.[2] Lugha hii inazungumzwa na takriban 95% ya wakazi wa nchi,[3] na idadi kubwa ya watu nchini Jibuti.[4]

Kufuatia kuanza kwa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Somalia miaka ya 1990, watu wanaoishi nje ya nchi wanaozungumza Kisomali waliongezeka kwa ukubwa, huku jumuiya mpya zaidi za wazungumzaji wa Kisomali zikiundwa katika sehemu za Mashariki ya Kati, Amerika Kaskazini na Ulaya.[2]

Tanbihi

hariri
  1. Saeed, John Ibrahim (1999). Somali. London Oriental and African language library. Amsterdam: J. Benjamins. ISBN 978-90-272-3810-8.
  2. 2.0 2.1 "Somali | Ethnologue Free". Ethnologue (Free All) (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-02-06.
  3. Sawaie, Mohammed (2005-12). "A Grammatical Sketch of Somali (review)". Language. 81 (4): 1004–1005. doi:10.1353/lan.2005.0200. ISSN 1535-0665. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help)
  4. Lecarme, Jacqueline; Maury, Carole (1987-01). "A software tool for research in linguistics and lexicography: Application to Somali". Computers and Translation (kwa Kiingereza). 2 (1): 21–36. doi:10.1007/BF01540131. ISSN 0884-0709. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help)

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kisomali kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.