Kiswaga Boniventura Destery

Kiswaga Boniventura Destery (alizaliwa Lugeye, Wilaya ya Magu, 8 Agosti 1974) ni mwanasiasa Mtanzania, mwanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM).

Amechaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Magu kwa miaka 20152020. [1] Amechaguliwa tena kwa mara ya pili kuwa Mbunge wa Jimbo la Magu miaka 2020-2025, huku akipenya kutoka katika kinyang'anyiro cha makada wa CCM 45 waliojitosa naye katika Ubunge.

Kiswaga alipata elimu yake ya msingi katika Shule ye msingi ya Salisima iliyoko katika Kijiji cha Lugeye, na baadaye elimu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari ya Bulima. Baadaye alipata mafunzo ya Uongozi na Biashara katika Chuo cha Uongozi kilichopoko Kijitonyama ambapo alitunukiwa astashahada ya Uongozi na utawaka wa fedha.

Kabla ya kuwa mbunge Kiswaga alichaguliwa kuwa Diwani kwa mara ya kwanza mwaka 2000, akiwa Diwani katika Kata ya Kitongosima iliyoko katika Tarafa ya Kahangara ndani ya Wilaya ya Magu, mkoa wa Mwanza.

Alihudumu kama Diwani kwa miaka 15, na mwaka 2005 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauari ya Wilaya ya Magu na kuandika historia ya kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri mwenye umri mdogo kuliko wote tangu Wilaya ya Magu ianzishwe.

Amewahi pia kushika nafasi mbalimbali katika Chama cha Mapinduzi(CCM)

Mwaka 2003-2008 alichaguliwa na kuingoza Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)Wilaya ya Magu akiwa ni Mwenyekiti wa Wilaya.

2012-2017 Alichaguliwa na kuwa Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa(NEC)

Halafu alijitosa katika kinyang'anyiro cha ubunge na kumwaga wasomi wakiwemo wahandisi na madaktari ambao walichuana naye. Na kuandika Historia ya kuwa mbunge wa nane wa Jimbo la Magu tangu lilipoanzishwa mwaka 1965.

Kiswaga nje ya siasa ni mfanyabiashara, Mwanzilishi na Mkurugenzi wa kampuni za Lugeye Investment na Lugeye Oil yaliyoko katika jiji la Mwanza.

Marejeo

hariri
  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017