Krak des Chevaliers

Krak des Chevaliers (tamka: krak de she-va-lyee; kwa Kiarabu: قلعة الحصن Qalaat al-Husn) ni ngome ya kihistoria nchini Syria ambayo imeandikishwa katika orodha ya urithi wa dunia. Inapatikana juu ya mlima kwa kimo cha mita 600, takriban katikati ya mji wa Homs na pwani ya Bahari Mediteranea. Ilijengwa wakati wa vita za misalaba kama miaka 800 iliyopita ikawa kituo muhimu cha wanajeshi wa misalaba kutoka Ulaya.

Ngome ya Krak des Chevaliers, Syria
Mahali pa Krak des Chevaliers nchini Syria

Historia hariri

Ngome ya kwanza ilijengwa huko na mtawala Mwislamu wa Aleppo. Askari Waislamu waliondoka wakati jeshi la vita ya kwanza ya misalaba lilipopita hapa.

Mnamo mwaka 1110 mtawala Mkristo wa Galilaya alituma watumishi wa kudumu walioanza kuimarisha ngome ya awali. Mnamo 1142 ilipitishwa mikononi mwa shirika la wanajeshi wa hospitali ya Mtakatifu Yohane walioendelea kuijenga.

Ngome hii ilikuwa kituo kikuu cha Shirika la Mtakatifu Yohane lililoweza kuitetea hadi mwaka 1271. Mwaka ule jeshi kubwa la Mamaluki wa Misri waliishambulia kwa nguvu na wateteaji wa mwisho walikabidhi ngome kwa maadui wakipata wenyewe nafasi ya kuondoka kwa usalama.

Ngome ilitengenezwa baadaye mara mbili, awali na Waarabu na katika karne ya 20 na Wafaransa waliotawala Syria kati ya vita kuu ya kwanza na vya pili.

Umuhimu hariri

Krak des Chevalier ni kati ya mifano bora ya usanifu wa ngome za Kiulaya na pia za Kiislamu za Enzi ya kati. Tangu mwaka 2006 imeandikishwa katika orodha ya UNESCO ya urithi wa dunia. Hadi vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria ilitembelewa na watalii wengi wa kimataifa.

Kutokana na mapigano ya vita hivyo ngome ilipata kiasi cha uharibifu.

Picha hariri