Kasoko ya Chicxulub
Kasoko ya Chicxulub (tamka chik-shulub) ni kasoko kubwa ya dharuba kwenye pwani ya rasi ya Yucatan katika Meksiko, iliyosababishwa na pigo la asteroidi miaka milioni 66 iliyopita. Inaaminiwa ya kwamba tukio hilo lilisababisha kuangamia kwa dinosauri pamoja na spishi nyingine nyingi Duniani.
Kasoko hii ina kipenyo cha zaidi ya km 180, hivyo ni kasoko kubwa ya tatu duniani iliyosababishwa na dharuba ya asteroidi (en:impact crater) [2] Asteroidi iliyogonga huko ilikuwa na kipenyo cha angalau km 10. Pigo hilo lilisababisha tsunami, kuwaka kwa moto katika sehemu nyingi za Dunia, matetemeko ya ardhi na kulipuka kwa volkeno nyingi. Kutokana na vumbi na majivu yaliyorushwa angani nuru ya jua ilizuiliwa na hivyo kilitokea kipindi kirefu cha giza na baridi kali kote duniani.[3]
Kasoko haionekani tena kwa macho au kutoka ndege maana mmomonyoko kwenye uso wa ardhi umeshasawazisha milima na kufukia shimo. Lakini vipimo vinaonyesha mabadiliko katika miamba ya eneo hilo na mabadiliko katika uga wa graviti ya eneo hili yanayotokana na densiti kubwa ya miamba pale ambako pigo lilikandamiza mwamba. Umri wa mwamba ulipimwa na kukadiriwa kuwa takriban miaka milioni 65 - 66. Umri huo unalingana na kupotea ghafla kwa spishi nyingi kote duniani jinsi inavyoonekana katika mabaki ya kisukuku.[4][5]
Marejeo
- ↑ "PIA03379: Shaded Relief with Height as Color, Yucatan Peninsula, Mexico". Shuttle Radar Topography Mission. NASA. Iliwekwa mnamo Oktoba 28, 2010.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Earth Impact Data Base: [1] Ilihifadhiwa 12 Februari 2010 kwenye Wayback Machine.
- ↑ Climate model simulations of the effects of the asteroid impact at the end of the Cretaceous, Brugger, J., G. Feulner, and S. Petri (2017), Baby, it's cold outside: Climate model simulations of the effects of the asteroid impact at the end of the Cretaceous, Geophys. Res. Lett., 44, 419–427, doi:10.1002/2016GL072241.
- ↑ Schulte, Peter; na wenz. (5 Machi 2010). "The Chicxulub Asteroid Impact and Mass Extinction at the Cretaceous-Paleogene Boundary". Science. 327 (5970). AAAS: 1214–1218. doi:10.1126/science.1177265. ISSN 1095-9203. PMID 20203042. Iliwekwa mnamo 5 Machi 2010.
{{cite journal}}
: Cite has empty unknown parameter:|coauthors=
(help); Explicit use of et al. in:|first=
(help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ *Rincon, Paul. "Dinosaur extinction link to crater confirmed", BBC, 2010-03-04. Retrieved on 2010-03-05.