Liberata Mulamula

Balozi wa Tanzania nchini Marekani aliwahi kuwa Waziri wa mambo ya nje na ushirkiano wa Afrika Mashariki

Liberata Mulamula (alizaliwa 10 Aprili 1956) ni mwanadiplomasia wa Tanzania alikuwa Waziri katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tangu Machi 2021 [1] hadi 2 Oktoba 2021[2]. Tangu mwaka 2015 alihudumu kama katibu mkuu wa wizara hiyo[3]. Aliwahi kuwa balozi wa Tanzania nchini Marekani pamoja na Meksiko [4] [5], aliwakilisha Tanzania pia kwenye Umoja wa Mataifa pamoja na Kanada na kati ya miaka 20062011 alikuwa katibu mtendaji wa Mkutano wa Kimataifa wa Kanda la Maziwa Makuu ya Afrika[6].

Liberata Mulamula

Rais Samia Suluhu Hassan
mtangulizi Palamagamba Kabudi

Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Meksiko
Rais Jakaya Kikwete
mtangulizi Mwanaidi Maajar

Mshauri wa rais
(Diplomasia)
Rais Jakaya Kikwete

Katibu Mtendaji wa ICGLR
aliyemfuata Ntumba Luaba

Balozi wa Tanzania nchini Kanada
Rais Benjamin Mkapa

utaifa Tanzanian
ndoa George
watoto 2
mhitimu wa Chuo Kikuu cha St. John's (New York City) (MA)
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Maisha binafsi

hariri

Liberata Rutageruka alizaliwa huko Muleba, mkoa wa Kagera. [7]

Alihitimu shahada ya uzamili katika somo la siasa kwenye Chuo Kikuu cha St. John’s, New York mwaka 1980 na pia kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mnamo 1989.

Ameolewa na George Mulamula na ana watoto wawili, Tanya na Alvin.

Marejeo

hariri

 

  1. ‘Sura’ tatu za uteuzi wa balozi Mulamula, gazeti la Mwananchi 02.04.2021
  2. President Samia reshuffles cabinet Archived 3 Oktoba 2022 at the Wayback Machine., gazeti Citizen tar. 02.10.2022
  3. "Balozi Mulamula". Michuzi Blog. 4 Mei 2015. Iliwekwa mnamo 4 Mei 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Kikwete picks new envoys". Mei 15, 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 13, 2013. Iliwekwa mnamo Agosti 8, 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Ambassador's Biography". Tanzaniaembassy-us.org. Embassy of Tanzania, Washington, D.C. Julai 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Agosti 1, 2013. Iliwekwa mnamo Agosti 8, 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-08-23. Iliwekwa mnamo 2021-04-02.
  7. Alumni of the Month: Liberata Rutageruka Mulamula, University of Dar es Salaam.
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Liberata Mulamula kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.