Open main menu

Kanisa la Wakaldayo

(Elekezwa kutoka Wakaldayo)

HistoriaEdit

Kanisa hilo linachanga historia moja na Kanisa la Asiria hasa hadi mwaka 1552, lilipotokea farakano kati yao, huku waliojiita Wakaldayo wakiungana na Kanisa Katoliki kama walivyotangulia kufanya wenzao kadhaa wa Cyprus mwaka 1445[4]

MuundoEdit

Kanisa hilo linaongozwa na Patriarki wa Babuloni, kwa sasa Louis Raphaël I Sako (kwa Kisiria: ܠܘܝܣ ܪܘܦܐܝܠ ܩܕܡܝܐ ܣܟܘ) aliyezaliwa tarehe 4 Julai 1948 na anayeishi Baghdad, Iraki.[5]

Chini yake kuna majimbo kati nchi hiyo, nyingine za Mashariki ya Kati na kwenye mtawanyiko uliotokana na waamini kuhama kwa sababu ya hali ngumu hasa ya vita na dhuluma: Iran, Siria, Uturuki, Lebanon, Misri, Kanada, Marekani, Australia na New Zealand n.k.

TanbihiEdit

  1. TQ & A on the Reformed Chaldean Mass. Iliwekwa mnamo 2009-02-07.
  2. Ronald Roberson. The Eastern Catholic Churches 2010. Catholic Near East Welfare Association. Iliwekwa mnamo Desemba 2010. Information sourced from Annuario Pontificio 2010 edition
  3. CNEWA - Chaldean Catholic Church
  4. Council of Florence, Bull of union with the Chaldeans and the Maronites of Cyprus Session 14, 7 Agosti 1445 [1]
  5. AP

Viungo vya njeEdit