Kihindustani

Kihindustani (pia: Kihindi-Kiurdu) ni lugha ya pamoja katika kaskazini ya Uhindi na Pakistan.

Neno "Hindustani" kwa maandishi ya Devanagari na Kiarabu.

Inapatikana kwa umbo sanifu tofauti katika nchi hizo: Kiurdu katika Pakistan na Kihindi katika India.

Kinahesabiwa kuwa kati ya lugha za Kihindi-Kiajemi ndani ya lugha za Kihindi-Kiulaya. Lugha za karibu ni pamoja Kipunjabi, Kisindhi, Kigujarati, Kimarathi na Kibengali.

Maandishi ni tofauti kila nchi, yaani upande wa Pakistan kinaandikwa kwa herufi za Kiarabu na upande wa Uhindi kwa herufi za Devanagari. Lakini kama lugha ya majadiliano hakuna tofauti. Sarufi ni sawa, lakini kuna kiasi cha tofauti katika msamiati hasa, katika lugha ya maandishi. Upande wa Kiurdu / Pakistan kuna maneno mengi zaidi yenye asili ya Kiarabu, Kituruki na Kiajemi. Upande wa Uhindi waandishi hutumia zaidi maneno yenye asili katika Kisanskrit.

Kabla ya ugawaji wa Uhindi ya Kiingereza mwaka 1947 majina kama Hindustani, Urdu, na Hindi yalikuwa na maana ileile na kutumiwa kwa mchanganyiko. Leo hii neno "Hindustani" bado hutumiwa kwa lugha inayozungumzwa kote Uhindi kaskazini na Pakistan, pia mara nyingi kwa ajili ya lugha ya Wahindi wanaokaa nje ya Uhindi tangu muda mrefu kwa mfano: "Fiji Hindi" na Hindustani ya Surinam.

Viungo vya njeEdit