Lusia wa Sirakusa
Lusia wa Sirakusa (maarufu kama Mtakatifu Lusia; 283 – 304) alikuwa msichana bikira na tajiri wa Siracusa, Sicilia, Italia visiwani ambaye alitetea imani yake ya Kikristo hadi kuuawa wakati wa dhuluma ya kaisari Dioklesyano.
Kadiri ya Injili, maisha yake yote alitunza taa yake inawaka ili kumlaki Kristo, Bwanaarusi wake, akamfia na kuingia pamoja naye kwenye arusi ya mbinguni, akafurahie milele nuru isitotua kamwe [1].
Anachorwa akishika mkononi sinia yenye macho yake aliyonyofolewa kabla hajauawa.
Kwa sababu hiyo anaheshimiwa tangu zamani kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 13 Desemba[2].
Tazama pia
haririTanbihi
haririViungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
- Jacobus de Voragine, Legenda Aurea: Archived 9 Desemba 2000 at the Wayback Machine. St. Lucy (e-text, in English)
- "Cara Santa Lucia..." Archived 9 Desemba 2013 at the Wayback Machine. (Kiitalia)
- "St. Lucy" from New Advent's Catholic Encyclopedia.
- Representations of Saint Lucy Archived 3 Aprili 2010 at the Wayback Machine.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |