Junipero Serra, O.F.M. (jina la kiraia lilikuwa Miquel Josep Serra i Ferrer; Petra, Majorca, Hispania, 24 Novemba 1713 - misheni ya San Carlos Borromeo de Carmelo, California, Hispania Mpya, leo nchini Marekani, 28 Agosti 1784) alikuwa mtawa, padri na mmisionari wa Kanisa Katoliki.

Junipero Serra alipokuwa na umri wa miaka 61 (1774).

Alianzisha misheni moja katika Baja California na nyingine 9 kati ya 21 za kwanza kati ya San Diego na San Francisco, Marekani. Walengwa wakuu wa misheni hizo walikuwa Waindio, ambao aliwainjilisha kwa lugha zao pamoja na kuwatetea kwa nguvu haki za maskini, bila kujali matatizo na magumu mengi[1].

Alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri tarehe 25 Septemba 1988, halafu na Papa Fransisko kuwa mtakatifu tarehe 23 Septemba 2015.[2]

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Julai[3] [4].

Sanamu ya Junípero Serra akiwa na Juaneño, mtoto Mwindio), Havana, Cuba.

Tazama pia hariri

Maandishi yake hariri

  • Writings of Junípero Serra, ed. and trans. by Antonine Tibesar, 4 vols. (Washington, D.C,. 1955-66).

Tanbihi hariri

  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/60125
  2. "Pope to Canonize ‘Evangelizer of the West’ During U.S. Trip". National Catholic Register. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-09-27. Iliwekwa mnamo 21 January 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
  3. Martyrologium Romanum
  4. "Patron Saints and their feast days". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-06-22. Iliwekwa mnamo 15 June 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.