Mabradha wa Shule za Kikristo
Mabradha wa Shule za Kikristo (kwa Kilatini: Institutum fratrum scholarum christianarum; kwa Kifaransa: Frères des écoles chrétiennes; kifupi: F.S.C.[1]) ni shirika lililoanzishwa kwa tabu nyingi na padri Yohane Baptista de La Salle (1651-1719) kwa ajili ya malezi ya kiutu na ya Kikristo ya vijana, hasa fukara, huko Reims (Ufaransa) mwaka 1680.
De La Salle aliingia kazi ya malezi taratibu, bila ya kukusudia, kadiri ya matukio na watu aliokutana nao.
Juhudi zake za kuanzisha shirika la mabradha tu kwa ajili ya kuendesha shule zilipata upinzani mkubwa kwa sababu ulikuwa mpango mpya.
Pia mbinu zake zilikuwa hazijazoeleka, kama vile kutumia lugha ya kawaida na kutodai ada yoyote.
Hata hivyo alifaulu kuanzisha mtandao wa shule nchini Ufaransa.
Mnamo Desemba 2023 watawa wa shirika hilo walikuwa 2,883 katika nchi 78, wakiongoza vituo vya elimu 1,154 vyenye wanafunzi 1,160,328.
Waliotangazwa watakatifu
haririTanbihi
hariri- ↑ Ann. pont. 2007, p. 1498.
Marejeo
hariri- Annuario pontificio per l'anno 2007, Libreria editrice vaticana, Città del Vaticano 2007. ISBN 978-88-209-7908-9.
- Bibliotheca Sanctorum (12 voll.), Istituto Giovanni XXIII nella Pontificia Università Lateranense, Roma 1961-1969.
- Mario Escobar (cur.), Ordini e congregazioni religiose (2 voll.), SEI, Torino 1951-1953.
- Guerrino Pelliccia e Giancarlo Rocca (curr.), Dizionario degli istituti di perfezione (10 voll.), Edizioni paoline, Milano 1974-2003.
- Giancarlo Rocca (cur.), La sostanza dell'effimero. Gli abiti degli ordini religiosi in Occidente, Edizioni paoline, Roma 2000.
- Maurice Hermans, La Casa Generalizia dei Fratelli delle Scuole Cristiane: 50 anni di storia, 1987.
- Georges Rigault, History of the Institute: The institute in Europe and in mission countries, Paris, Librairie Plon, 1951.
Viungo vya nje
hariri- http://www.lasalle.org Tovuti rasmi
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mabradha wa Shule za Kikristo kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |