Kaunti ya Machakos
Kuhusu mji, soma Machakos
Kaunti ya Machakos | |||
---|---|---|---|
Kaunti | |||
Ofisi ya gavana wa Machakos | |||
| |||
Machakos County in Kenya.svg Kaunti ya Machakos katika Kenya | |||
Coordinates: 01°14′S 37°23′E / 1.233°S 37.383°E | |||
Nchi | Kenya | ||
Namba | 16 | ||
Ilianzishwa | Tarehe 4 Machi, 2013 | ||
Ilitanguliwa na | Mkoa wa Mashariki | ||
Makao Makuu | Machakos | ||
Miji mingine | Kangudo, Matuu, Kithimani, Athi River | ||
Gavana | Dkt. Alfred Mutua, CBS | ||
Naibu wa Gavana | ENG. Francis Maliti Wambua | ||
Seneta | Boniface Mutinda Kabaka | ||
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa) | Joyce Kamene | ||
Bunge la Kaunti | Bunge la Kaunti ya Machakos | ||
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa | 40 | ||
Maeneo bunge/Kaunti ndogo | 8 | ||
Eneo | km2 6 042.7 (sq mi 2 333.1) | ||
Idadi ya watu | 1,421,932 | ||
Wiani wa idadi ya watu | 235 | ||
Kanda muda | Saa za Afrika Mashariki (UTC+3) | ||
Tovuti | http://www.machakosgovernment.com/ |
Kaunti ya Machakos ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.
Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 1,431,932 katika eneo la km2 6,042.7, msongamano ukiwa hivyo wa watu 235 kwa kilometa mraba[1].
Makao makuu yako Machakos. Inatarajiwa kuwa na mji wa Konza ambao ndio mji wa kwanza wa teknohama katika Afrika Mashariki.
Jiografia
haririKaunti ya Machakos inapakana na Nairobi, Kiambu, Murang'a (magharibi), Embu (Kaskazini), Kitui (mashariki), Makueni na Kajiado(kusini). Tabianchi ya Kaunti ya Machakos ni nusu kavu. Ina mandhari yenye vilima[2]. Udongo katika maeneo mengi ni udongo wa mfinyanzi ulio mwekundu. Hata hivyo, kuna mito ambayo huchimbwa mchanga haramu. Jambo hili huharibu mandhari kwa kukausha mito.
Mto Tana na Mto Athi hupitia katika kaunti hii. Bwawa la Masinga liko kaskazini katika mpaka wa Machakos na Embu.
Kiwango cha ardhi kilicho misitu ni 7.6%. Vyanzo vya maji katika kaunti ni Vilima vya Iveti, Muumandu, Kalimanzalu and Kiima Kimwe.
Machakos hupata misimu miwili ya mvua, Oktoba hadi Disemba na Machi hadi Mei. Maeneo yaliyo na vilima hupata mvua mingi, kiwango cha mm 1000, kuliko maeneo kavu ambayo hupata mvua ya kiwango cha mm 500. Mwezi wa Julai huwa na baridi zaidi.
Utawala
haririKaunti ya Machakos imegawanywa katika maeneo bunge yafuatayo[3]:
- Athi River 322,499
- Kalama 54,462
- Kangundo 97,917
- Kathiani 111,890
- Machakos 170,606
- Masinga 148,522
- Matungulu 161,557
- Mwala 181,896
- Yatta 172,583
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
- ↑ "Machakos Government - Official Website". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-04-09. Iliwekwa mnamo 2018-04-18.
- ↑ "Machakos County". Iliwekwa mnamo 2018-04-18.
{{cite web}}
: Text "County Trak Kenya" ignored (help) - ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kaunti ya Machakos kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |