Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

  • usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
  • usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
  • usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
  • usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
  • do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing them themselves.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

--Mr Accountable (majadiliano) 11:53, 24 Novemba 2009 (UTC)Reply

Samson Maosa Nina furaha tele kuwa mmoja kati ya wachangiao kuikuza wikipedia ya Kiswahili kupitia kwa Shindano linaloendelea la swahili wikipedia Challenge. Nitajitahidi kuona kwamba ninatafsiri makala mengi niwezavyo na kuhariri makala mapya. Sipo hapa kwa ajili ya shindano, nitakuwa hapa daima kuikuza wikipedia kwa lugha ya Kiswahili. Nawashukuru nyote wanawikipedia kwa kunipa fursa hii murwa ya kujiendeleza. Karibu sana - Bwana kama kweli utaweza itakuwa ni safi sana. Je umeona nilichoandika kwenye ukurasa wako wa submissions chini ya "Ruiru"?? Basi endelea na ubarikiwe!!! --Kipala (majadiliano) 19:57, 10 Januari 2010 (UTC)Reply

Picha:Lornalaboso.jpg

hariri

Hi, thank you for uploading pictures to the Wikipedia! Please see Msaada:Picha for information about copyright and picture categories (for example Jamii:Picha za watu). Thanks again. --Mr Accountable (majadiliano) 15:27, 11 Januari 2010 (UTC) Asante sana Mr. Accountable. Naelekea huko saa hii. Asante tena. Maosa Samson.Reply

Kisii, Kenya

hariri

Uliona ukurasa wa majadiliano wa makala ile? --Kipala (majadiliano) 20:24, 11 Januari 2010 (UTC) Nishayapitia. Nimefanya marekebisho ifaavyo. Asante sana. Samson Maosa (majadiliano)Reply

kutunga kurasa za jamii

hariri

Ndugu Samson, salaam! Nimefurahi kuona kwamba umepanua kazi yako, siyo makala tu bali hata vigezo na kurasa za jamii. Sasa upande wa jamii, naomba usiandike maelezo ya jamii humo. Angalia jinsi ilivyoandikwa kwa Kiingereza. Taja jamii ya juu tu, k.m. [[Jamii:Mavazi ya miguu]], halafu rejea kwa wikipedia nyingine, k.m. [[en:Category:Shoes]]. Basi. Asante, na wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 20:21, 16 Januari 2010 (UTC)Reply

Asante sana ndugu BT kwa kunirekebisha. Nitayarekebisha makosa haya. Kupotea njia ndiko kujua njia, ndivyo walivyosema wavyele.

Samson

Ee, ndivyo ilivyo kweli. Au wanavyosema pia, kufanya kosa siyo kosa, kurudia kosa ndilo kosa. Nikushauri upande mwingine pia. Ukijibu kwenye ukurasa wa majadiliano, uanze mstari mpya na nukta mbili hivi, :. Halafu ukitia sahihi, uandike ~~~~ tu. Hii ni "code" kwa ajili ya jina lako la utumiaji pamoja na tarehe na saa za jibu. Kuishi ni kusaidiana. Tusonge mbele! --Baba Tabita (majadiliano) 20:52, 16 Januari 2010 (UTC)Reply
Kweli palipo na watu wazima hapaharibiki jambo. Nimeyasoma mengi kutoka kwako na masogora wengine! Bado ninazidi kusema shukrani. Unaonaje nilivyojibu hili sasa? Mola akuzidishie baraka. Coolsam726 (majadiliano) 21:01, 16 Januari 2010 (UTC)Reply

Who Am I?

hariri

Salam, Samson. Umeiona hiyo makala ya Who Am I? ? Nimeongezea kitu kama sanduku la habari la filamu na mengineyo. Pia, nimebadilisha mifumo ya uitaji wa filamu na kadhalika. Ukiwa una swali lolote kuhusu majedwali ya muziki na filamu, basi niulize na nitakujibu! Katika field ya muziki na filamu, niko makini kinoma. Basi kila la kheri!--MwanaharakatiLonga 06:46, 20 Januari 2010 (UTC) Reply

Asante sana Ndugu Longa kwa mabadiliko hayo. Makala sasa yavutia kweli! Wewe ni gwiji wa mambo hayo. Nina maswali ndio lakini hebu kwanza niyapitie mabadiliko yako angalau nijifunze kutoka kwako. Hatimaye nikiwa na swali nitakuandikia. Asante tena. Coolsam726 (majadiliano) 10:45, 20 Januari 2010 (UTC)Reply
Pole! Mimi si Ndugu "Longa". Niite tu Muddy au Muddyb! Hiyo ni michezo ya kubadilisha signature ije kwa mtindo gani! Si kitu. Tazama mabadiliko halafu unieleze! Kila la kheri.--MwanaharakatiLonga 11:26, 20 Januari 2010 (UTC)Reply

Mwongozaji wa filamu

hariri

Salam, Cool! Eti, si unajua namna mtu anaye-direct film kwa Kiswahili wanamwitaje? Ni tumaini langu ndiyo, lakini pia si mbaya tukiambiana tena! Film director wanamwita "mwongozaji wa filam" - na sentence kama "film directed by Coosam726 on - na -... Yaani, filamu iliongozwa na... Na si ilielekezwa na... Kama kinyume vile? Haya, sijui sana, lakini tusipishane kama jinsi tulivyoongea kwenye e-mail! Kila la kheri..--MwanaharakatiLonga 06:16, 25 Januari 2010 (UTC) Reply

Ningepataje kujua bwana! Nimegundua tu saa hii wakati nikipitia source code ya Filamu na nimerekebisha kosa hilo katika makala ya mwisho niliyoikabidhi. Sasa nimejua Bwana na asante sana Producer. Nitajaribu kurekebisha. Je, Umeona majadiliano yako? Nilikuuliza kuhusu sanduku la Mwigizaji wa filamu (Film Actor). Kila la heri pia. Coolsam726 (majadiliano) 06:25, 25 Januari 2010 (UTC)Reply
Pole! Lakini pia sichoki hata kidogo. Eti nani alijua mwenyewe yote bila hata kudokezwa? Kipala ndiyo mwongozo wangu wa awali. Labda na wewe miye huenda nikawa mwongozo wako wa sasa! Basi tushirikiane kwa lolote ulitakalo (kiwiki-wiki) halafu tuone itakuwaje! Hebu songesha!--MwanaharakatiLonga 06:40, 25 Januari 2010 (UTC)Reply
Ninatumai kujifunza mengi kutoka kwako. Shekrani sana. Walisema Umoja ni Nguvu.Coolsam726 (majadiliano) 06:45, 25 Januari 2010 (UTC)Reply

Jamii

hariri

Salam, Samson. Kuna ubaya nikikueleza na kukumbusha kuhusu jamii? Kila jamii inatakiwa iwe na jamii ya chini. Kwanini ninasema jamii ya chini? Jamii ya juu na jamii ya chini ni mfumo wa kutaja jamii kuu na ndogo. Yaani hivi, jamii ya "Wanamuziki wa Kenya" ipo chini ya jamii ya Watu wa Kenya. Mfano:

Ukianzaisha jamii ni lazima chini yake uweke kitu. Kama jinsi ulivyoandika katika Jamii:Wilaya ya Dondo:

Jamii:Jiografia ya Kenya.

Ukiwa hujaelewa, nitakueleza vizuri!--MwanaharakatiLonga 07:41, 26 Januari 2010 (UTC) Reply

Tena, angala mfano huu:

Utaona jinsi nilivyoweka, kaka.--MwanaharakatiLonga 07:48, 26 Januari 2010 (UTC) Reply

Nimekuelewa kabisa Producer. Asante sana kwa ujuzi. Nitaziongeza jamii hizo kuu sasa.Coolsam726 (majadiliano) 08:16, 26 Januari 2010 (UTC)Reply

Kigezo:Siasa ya Kenya

hariri

Salam tena! Nimeanzisha hicho kigezo, lakini sijakimaliza. Je, unaweza kukimalizia? Wako,--MwanaharakatiLonga 07:59, 26 Januari 2010 (UTC)] Reply

Itakuwa furaha yangu kubwa kukiendeleza kigezo hicho.Coolsam726 (majadiliano) 08:17, 26 Januari 2010 (UTC)Reply
Wow! Imekaa poa sana. Lakini Kigezo:Politicsboxend - hakitafisiriwi kabisaaaa! Kwa sababu hicho ni kama kiungo fulani kwa viungo maalumu! Hivyo hakina ulazima wa kutafsiriwa, kaka! Halafu? Eti, kweli wewe ni native wa Kiingereza? Basi ni hayo tu!--MwanaharakatiLonga 09:03, 26 Januari 2010 (UTC)Reply
Haha. Mimi si native wa Kiingereza. Mimi ni native wa Kikisii na lugha hizi zote nimejifunza nikikua. asante lakini.Coolsam726 (majadiliano) 09:15, 26 Januari 2010 (UTC)Reply

makala zihitajizo habari

hariri

Ndugu Samson, salaam! Wakati wa shindano, makala nyingi zimeanzishwa bila kuwekewa yaliyomo hata kidogo, nasi wanawikipedia hatukuwa na nafasi ya kurekebisha sana. Kwa hiyo sasa, naomba tusaidiane kusawazisha hizo makala. Kwa mfano, ungeweza kuanza kwa kuangalia orodha ya makala bila jamii. Bila shaka utagundua kadhaa ambazo ni duni, labda yenye maneno mawili matatu tu. Ndivyo nilivyogundua k.m. na makala ya Henri Fayol, mhandisi Mfaransa wa karne ya 19. Sasa ukiangalia mabadiliko niliyoyaingiza utapata mambo ya msingi ya wikipedia. K.m. naingiza kigezo cha {{DEFAULTSORT}} kwa ajili ya orodha ya makala katika jamii ifuate alfabeti vizuri. Tena naingiza jamii za miaka ya kuzaliwa (k.m. [[Jamii:Waliozaliwa 1841]]) na ya kufariki (k.m. [[Jamii:Waliofariki 1925]]). Pia, ikiwa ni makala fupi bila maelezo mengi, naingiza kigezo cha {{mbegu-mtu}} (yaani kama ni mtu). Hatimaye, naingiza kiungo kwa wikipedia ya Kiingereza (k.m. [[en:Henri Fayol]]) ambapo naweza kupata code kwa picha ya mtu (k.m. [[Image:Fonds henri fayol.jpg|thumb|right|Henri Fayol]]) pamoja na habari nyingine. Nitashukuru kwa msaada wako katika kuboresha makala mpya zilizoachwa duni. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 10:58, 2 Februari 2010 (UTC)Reply

Itakuwa furaha yangu BT. Nitafanya jitihada kubwa kuyarekebisha makala mengi niwezavyo. Asante sana kwa mwaliko huo. Itakuwa fursa yangu kuonyesha shukrani kwa mengi niliyoyasoma hapa. Heri na fanaka kwako.Coolsam726 (majadiliano) 12:55, 2 Februari 2010 (UTC)Reply

angalia majadiliano na ukurasa wa historia

hariri

Unisamehe nikiendelea kuandika kuhusu usafishaji wa wikipedia baada ya shindano. Nimefurahi sana kuona jinsi ilivyokua wikipedia yetu. Sasa lakini, tukiendelea kuboresha makala zilizoongezeka, tuwe makini. Kabla hatujaongeza au kurekebisha habari za makala fulani, lazima tuangalie majadiliano na ukurasa wa historia ya makala hiyo. Angalia k.m. makala ya uchumi. Ukiihariri bila kuangalia majadiliano yake wala historia yake, inawezekana utaongeza kazi ya baadaye kwa vile tafsiri za shindano zilizofuta makala za zamani (pamoja na jamii na interwiki zake) hazijaunganishwa. Nitaendelea kutafuta makala kama hiyo na kuziandikia katika majadiliano yake. Kwa ajili ya kuunganisha tafsiri mbili au zaidi, labda itasaidia ukifungua zote, kila moja katika dirisha lake, na kunakilisha sehemu za makala za zamani kwenda katika makala ya sasa. Pole na kazi. Na asante kwa kazi yako. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 12:58, 2 Februari 2010 (UTC)Reply

Remarking my articles

hariri

I am so heartbroken. I worked hard for this laptop and just when I thought I was there, it seems now i have a long way to go and I now only depend on God in order to appear among the top 5. I thought what is displayed by one judge on my page has been scrutinized thoroughly and is final!! How did this happen?! Somebody please tell me!!!Coolsam726 (majadiliano) 04:03, 3 Februari 2010 (UTC)Reply

Salam, Samson! What makes you worry about? Jamani, wewe ndo mshindi wa kwanza jamani. So, don't be heartbroken again. Please trust me. Halafu? Jamani hii si nzuri hata kidogo (likitokea jambo la kuweka mambo sawa) nyie mwaanza kulalamika kama mwatolewa nafsi. Khe! Jamani hatwendi hivyo!!! Ili ukue, unatakiwa uwe na vitu kama hivi (ukoasiaji wa kimakala na kadhalika), lakini sio kukulupuka tu jamani eeeh! Kwa jinsi ninavyoona mimi na kwa hesabu ya makala zako zote ninapata kama 240... na kadhaa hivi, na kukufanya kuwa mshiriki wa kwanza kuwa na maxi nyingi kupita wote! Hapo je unasemaje? Sam, nina kuamini - nini tena lawama? Haya, wa pili katika hao ni hadi sasa ni Abbas Mahmoud (sijui kuhus Kandyzo ambaye anaonekana kuandika makala nyingi naye). Wengine ni kama Maria Alphonce na... Basi Samoson hongera!!! Karibu sana katika Wikipedia. Wako,--MwanaharakatiLonga 07:14, 3 Februari 2010 (UTC)Reply
Haya! Unadhani kwamba huna haki ya kulalamika pindi uonapo kitu kama kile? Hata kama ningekuwa miye, basi ningelalama! Lakini pia sikupenda kufanya vile, ila ilinibidi!!! Ni tumaini langu kuendelea kuchangia kwa furaha... Bado laptop ni yako baba kama ulivyosema hehehehehehe... You're almost weep out, man. Lakini pia tuendelee kuchangia hata baada ya shindano kwisha. Tena tutakuwa na uchaguzi wa kukabidhi watu wapya madaraka. Watu hao ni pamoja na Wewe, Limoke, Abbas, Kandyzo, na wengineo watakaotaka kubakia kwenye Wikipedia yetu! Je, hii ni shwari kwako? Basi twende kazi! Nikiwa ninatokea Dar es Salaam, Tanzania, niite Muddyb au,--MwanaharakatiLonga 10:00, 3 Februari 2010 (UTC)Reply
Hehehe... Wanifurahisha sana Mwanaharakati. Ninakubali nina haki ya kulalamika lakini pia wajua si vyema mtu kulalama ovyo ovyo na hiyo si tabia yangu kamwe, ndiyo maana nikaamua kujirekebisha kwa kuomba msamaha. Asante sana kwa yote. Nitapenda sana kubakia kwa Wikipedia, kwa hivyo kwangu hayo ni shwari kabisa.

Basi nami nikitokea Magharibi mwa Kenya, una hiari ya kuniita Sam au=>Coolsam726 (majadiliano) 10:33, 3 Februari 2010 (UTC)Reply

BAADA YA SHINDANO

hariri

Naam, baada ya shindano na kimya kifupi, Sam arejea tena. Wakati huu si kuwapa wenzake usiku usio na usono katika shindano, bali kuiendeleza Wikipedia yetu kadiri niwezavyo.

Pole kwa kimya changu lakini zilikuwa harakati za kufuailia tuzo langu na kujitayarisha kurejea shuleni. Katika mkutano na Google na Wikimedia nilijaaliwa kuonana na Erik Möller, Kiongozi Mkuu wa Mradi wa Wikimedia na mwenzake Frank, na vile vile Christine Moon na Angela wa Google. Pia nilikutana ana kwa ana na Dennis Gikunda, Meneja wa ustawi wa Kinyumbani wa Google katika Afrika. Pia asiyesahaulika ni Oliver Stegen: Ndio, Baba Tabita mwenyewe al maarufu BT. Hata hivyo nilifika nikiwa nimejelewa kwa hivyo nina huzuni kuwa sikupata fursa ya kuongea naye!! Niliona akiniangalia na macho ya kudadisi, haikosi hakujua ni Samson, lakini alishuku kuwa ni yeye.

Licha ya hao, ilikuwa fahari yangu kuburudika pamoja na washindi wengine kama Kamero, Abbas, Ivermarc, Xelawafs, Limoke, Jakibiro, Kosgey na wengineo (Kandyzo hakuonekana siku hiyo)

Tuyaache hayo. Sasa na iwe mwanzo basi vile Christine alisema. Tuliahidi kubaki papa hapa na sasa tumekuja kutimiza ahadi. Waswahili na wapate ujuzi kwa utele. Basi, iwapo una jukumu lolote kwangu, niarifu na nitalishughulikia kadiri nijaaliwavyo.

Pokea salamu tele kutoka kwa familia yangu ambao wana furaha kuona maendeleo ya mwana na ndugu yao.... Hapa ni Maghaaribi mwa Kenya; ukipenda Mkoa wa Nyanza, ukipenda zaidi Kisii.

Coolsam726 (majadiliano) 05:52, 17 Machi 2010 (UTC)Reply

Salam tena na karibu tena! Haya, naona toto la Maosa kume-mchea ili aanze vimbwanga vyake. Kwa mpango mzima wa kuandika makala sijui wewe unapendelea kuandika masuala gani? Binafsi najijua kama ni mpenzi wa muziki na filamu! Katika uga hizo nimejikita vya kutosha!!! Basi si ni afadhali tuambizane mwenzangu umelalia upande gani. Hii inarahisisha kutoa miongozo thatbiti kiusaidizi. Hebu nieleze - halafu tuangalie inakuwaje? Salam hizi zinatokea Buguruni, Ilala, Dar es Salaam, Tanzania! Niite Muddyb au,--MwanaharakatiLonga 06:19, 17 Machi 2010 (UTC)Reply
Basi hapo ukanipata. Ninapenda muziki na filamu sana, ingawa sina ujuzi mwingi huko. Kando na hayo, ya teknolojiaa pia hayanipiti. Hizo ndizo nyanja ninamotaka kujikita zaidi, isimaanishe sitahariri kuhusu maswala mengine. Salamu nazipokea.

Coolsam726 (majadiliano) 06:25, 17 Machi 2010 (UTC)Reply

Hahahaha! Kumbe! Hata mimi huandika masuala mengineyo! Lakini sana-sana ni muziki na filamu. Basi ukianzisha nami nitasonga. Hebu songesha!--MwanaharakatiLonga 06:30, 17 Machi 2010 (UTC)Reply
Vivyo hivyo mhibu. Nilishayafulia nguo wakati wa shindano, sasa nitajitoza humo mzima mzima niogelee.
Maosa, salam! Twende kazi - wacha rundo la maneno mtu wangu! Cheers.--MwanaharakatiLonga 05:41, 6 Aprili 2010 (UTC)Reply

makala ya Rais wa Afrika Kusini

hariri

Ndugu Sam, salaam! Sasa mwezi mzima umepita tangu umeahidi kuishughulikia makala ya Rais wa Afrika Kusini. Pole ukiwa huna nafasi. Je, lakini, tufanyeje? Bila shaka tusonge mbele. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 12:39, 6 Mei 2010 (UTC)Reply

Samahani sana BT. Wajua tena shughuli za kurudi shuleni zilivyo. Nilikuwa nimebanwa sana. Hata hivyo, ukurasa u tayari na utauona kwa wiki hivi punde.

Nashukuru kwa kumbusho.74.86.222.73 16:40, 6 Mei 2010 (UTC)Reply

Article requests

hariri

Hi! Do you do article requests?

If so, would you mind making stubs in Swahili of the following?

Also, are you in the Nairobi area? If so, do you do photo requests? I would like to get photos of some buildings in and around JKIA.

Thanks, WhisperToMe (majadiliano) 07:33, 23 Mei 2011 (UTC)Reply

Hi, thanks for your request. It will be my pleasure to find time to translate the articles when I can, and I will notify you. Coolsam726 (majadiliano) 00:52, 4 Juni 2011 (UTC)Reply
Alrighty - I look forward to the articles :) WhisperToMe (majadiliano) 06:21, 5 Juni 2011 (UTC)Reply

Hi again! Have you had a chance to start any of these articles? Thanks WhisperToMe (majadiliano) 00:50, 12 Septemba 2011 (UTC)Reply

Are you still active? WhisperToMe (majadiliano) 03:23, 19 Agosti 2013 (UTC)Reply