Kassim Majaliwa

(Elekezwa kutoka Majaliwa Kassim Majaliwa)

Kassim Majaliwa (* 22 Disemba 1960) ni mwanasiasa nchini Tanzania. Alikuwa mbunge wa jimbo la Ruangwa tangu mwaka 2010 akigombea kwa CCM.

Waziri Mkuu Majaliwa

Tarehe 19 Novemba 2015 aliteuliwa na rais John Magufuli kuwa waziri mkuu wa serikali ya awamu ya tano nchini Tanzania.[1]

Aliwahi kushika vyeo vya naibu waziri wa utawala wa mikoa na serikali ya mitaa katika ofisi ya waziri mkuu tangu mwaka 2010[2] [3]na mkuu wa mkoa wa Lindi kuanzia 2006 hadi 2010.

Majaliwa ni mwenyeji wa Mnacho katika Wilaya ya Ruangwa aliposoma shule ya msingi kati ya mwaka 1970 hadi 1976. Akaendelea kusoma kwenye Shule ya Sekondari Kigonsera hadi 1980. Miaka 1984-1986 alifanya kazi ya ualimu huko Lindi na tangu 1988 aliajiriwa na wizara ya elimu. Mwaka 1991 akajiunga na chuo cha ualimu Mtwara akaendelea na masomo ya digrii ya kwanza kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, masomo ya digrii ya pili kwenye Chuo Kikuu cha Stockholm (Uswidi) aliyomaliza 1999. Mwaka 2000 alipewa kazi ya Mkuu wa Wilaya.

Ni mpenzi wa michezo ya klabu za Tanzania na ni shabiki wa Simba S.C..

Marejeo Edit

  1. JPM names Kassim Majaliwa Prime Minister. THE CITIZEN. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-06-11. Iliwekwa mnamo 19 November 2015.
  2. Member of Parliament CV. Parliament of Tanzania. Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-07-22. Iliwekwa mnamo 24 February 2013.
  3. Taaarifa juu ya uteuzi wa Majaliwa kuwa Waziri mkuu katika gazeti la Mwananchi, 19 Novemba 2015. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-05-15. Iliwekwa mnamo 2015-11-19.
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kassim Majaliwa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.