Malkia wa Sheba
Malkia wa Sheba (kwa Kiebrania מַלְכַּת שְׁבָא malkaṯ shəḇāʾ; kwa Kiarabu: ملكة سبأ) ni mhusika anayetajwa kwa mara ya kwanza katika Biblia ya Kiebrania (1 Fal 10:2, 2 Nya 9). Katika taarifa hiyo, anaongoza msafara wa zawadi za thamani kwa Mfalme Sulemani wa Israeli. Taarifa hiyo imepitia ufafanuzi wa kina wa Kiyahudi, Kiislamu na Kiethiopia. Imekuwa chanzo cha hadithi zilizoenea katika nchi za Mashariki ya Kati. [1]
Wanahistoria wa leo wanaona "Sheba" kuwa ufalme ule unaoitwa pia "Saba" kusini mwa Uarabuni kwenye maeneo ya Yemen leo. Kuwepo kwa malkia huyo kunabishaniwa kati ya wanahistoria. [2]
Katika Biblia
haririMalkia wa Sheba anatajwa katika vitabu vya Wafalme na Nyakati lakini jina lake halitajwi. Kufuatana na 1 Fal 10 aliwahi kusikia habari za mfalme Suleimani akaja Yerusalemu "kumjaribu kwa maswali magumu" na "wafuasi wengi sana, na ngamia wachukuao manukato, na dhahabu nyingi sana, na vito vya thamani; alipomfikilia Sulemani, akazungumza naye mambo yote aliyokuwa nayo moyoni". Sulemani alijibu maswali yake wakabadilishana zawadi, kisha akarudi katika nchi yake. [3] [4]
Katika Agano Jipya anatajwa kama "Malkia wa Kusini“ atakayetokea kwenye siku za mwisho wa Dunia akitoa ushuhuda kuhusu watu wakati wa hukumu (Mt 12:42; Lk 11:31).
Mapokeo ya Kiyahudi
haririKwa Yosefu Flavius anatajwa kama "malkia wa kusini" na malkia wa Uhabeshi (Ethiopia) aliyeleta mbegu za uvumba hadi Uyahudi. (Antiquitates Judaicae 2:249, 94 n. Chr.).
Katika andiko la Targum Sheni (takriban karne ya 8 BK) kuna simulizi la Suleimani ambaye anatawala pia wanyama, na ndege mmoja anamletea habari za malkia tajiri sana aliyeko Sheba akamtumia barua ya kumwalika. Yule malkia hatimaye anakuja Yerusalemu. Akifika kwenye jumba la kifalme anakuta sakafu ya kioo akifikiri ni maji, kwa hiyo anavuta gauni yake juu. Hivyo Suleimani anaweza kuona nywele kwenye miguu yake. Malkia anampa Suleimani vitendawili ili kupima hekima yake.[5][6][7] [8][9][10]
Mapokeo ya Kiethiopia
haririKatika mapokeo ya Ethiopia malkia huyo anatokea katika nchi hiyo na jina lake ni Makeda. Habari zake ni sehemu ya masimulizi katika Kebra Negast. [11][12][13] Akitembelea Yerusalemu anazaa mtoto na Suleiman na mtoto huyu ndiye Menelik I ambaye katika historia ya Kebra Negast ni baba wa wafalme wote wa nasaba ya Suleimani katika Ethiopia[14].
Katika masimulizi ya Waethiopia, Mfalme Suleimani alitafuta wafanyabiashara kutoka pande zote za Dunia, ili kununua vifaa kwa ujenzi wa Hekalu la Yerusalemu. Miongoni mwao alikuwa Tamrin, mfanyabiashara mkuu wa Malkia Makeda wa Ethiopia. Baada ya kurudi Ethiopia, Tamrin alimwambia malkia juu ya mambo ya ajabu aliyoyaona huko Yerusalemu, na juu ya hekima na ukarimu wa Suleimani, ambapo aliamua kumtembelea Sulemani. Alikaribishwa kwa uchangamfu, akapewa jumba la makao, na kupokea zawadi kubwa kila siku. Sulemani na Makeda walizungumza kwa hekima nyingi, na kufundishwa naye, akageuka na kuwa Myahudi. Kabla hajaondoka, palikuwa na karamu kubwa katika jumba la mfalme. Makeda alikaa katika jumba la kifalme usiku kucha, baada ya Sulemani kuapa kwamba hatamdhuru, huku akiapa kwa kujibu kwamba hatamwibia. Kwa kuwa milo ilikuwa ya viungo, Makeda aliamka akiwa na kiuu usiku na akaenda kunywa maji, wakati Sulemani alipotokea, akimkumbusha juu ya kiapo chake. Akajibu: "Puuza kiapo chako, niruhusu tu ninywe maji." Usiku huohuo, Sulemani aliota ndoto kuhusu jua likichomoza juu ya Israeli, lakini kwa kutendewa vibaya na kudharauliwa na Wayahudi, jua lilisonga kuangaza Ethiopia na Roma. Sulemani akampa Makeda pete kama ishara ya imani, kisha akaondoka. Akiwa njiani kuelekea nyumbani, alijifungua mtoto wa kiume, ambaye alimpa jina la Baina-leḥkem (yaani bin al-ḥakīm, "Mwana wa Mwenye Hekima", baadaye aliitwa Menilek). Baada ya kijana kukua Ethiopia, alienda Yerusalemu akiwa amebeba pete na kupokelewa kwa heshima kubwa. Mfalme na watu walijaribu bila mafanikio kumshawishi abaki. Sulemani aliwakusanya wakuu wake na akatangaza kwamba atamtuma mtoto wake wa kwanza wa kiume huko Ethiopia pamoja na wazaliwa wao wa kwanza. Aliongeza kuwa alikuwa anatazamia mtoto wa tatu wa kiume, ambaye angemwoa binti mfalme wa Roma na kutawala Roma ili ulimwengu wote utawaliwe na uzao wa Daudi. Kisha Baina-lehkem akatiwa mafuta na Sadoki kuwa kuhani mkuu, akapokea jina jipya Daudi. Kabla ya kuondoka, wana wa makuhani walikuwa wameiba Sanduku la Agano, baada ya kiongozi wao Azarya kutoa dhabihu kama alivyoamriwa na malaika wa Mungu. Kwa maombolezo mengi, msafara huo uliondoka Yerusalemu kwa gari la kukokotwa na upepo lililoongozwa na kubebwa na malaika mkuu Mikaeli. Baada ya kufika kwenye Bahari ya Shamu, Azarya aliwafunulia watu kwamba Sanduku la Agano lenye amri 10 liko pamoja nao. Daudi aliomba kwa Sanduku na watu wakafurahi, kuimba, kucheza, kupiga tarumbeta na filimbi, na kupiga ngoma. Sanduku lilionyesha nguvu zake za miujiza wakati wa kuvuka Bahari yenye dhoruba, na wote walifika bila kujeruhiwa. Sulemani alipojua kwamba Sanduku lilikuwa limeibiwa, alimtuma askari wa farasi kuwafuata wezi hao na hata akawakimbiza, lakini hakuna aliyeweza kuwakamata. Sulemani alirudi Yerusalemu na kuwaamuru makuhani kuficha wizi huo na kuweka nakala ya sanduku kwenye Hekalu, ili mataifa ya kigeni yasiweze kusema kwamba Israeli imepoteza umaarufu wake. [15]
Mapokeo ya Kiislamu
haririMalkia wa Sheba anatajwa katika Kurani katika sura ya 27, aya 22-44[16]. Hadithi yake inafanana na mapokeo ya Kiyahudi. Ndege anamletea Suleimani habari za malkia katika nchi ya mbali anayeabudu Jua. Sulemani anatuma barua na kumwalika Malkia wa Sheba. Malkia anawauliza washauri wake wakuu ni hatua gani zichukuliwe. Anatangulia kutuma mabalozi kuwasilisha zawadi kwa Mfalme Sulemani. Anakataa zawadi hiyo, akitangaza kwamba Mwenyezi Mungu hutoa zawadi bora zaidi na kwamba mabalozi ndio pekee wanaofurahishwa na zawadi hiyo. Kisha Malkia anafanya mipango ya kumtembelea kwenye kasri lake. Hapa malkia anakiri imani yake kuwa amegeukia kwa Allah. Mwishoni maneno ya Qurani yanarudia hadithi jinsi malkia anapita kwenye sakafu anayoona ni maji na kuinua gauni yake.
Katika mapokeo yaliyotokea baada ya Kurani, jina la malkia hutajwa kuwa "Bilkis" (Kiar. بلقيس)[5].
Baadhi ya wafasiri wa Kiislamu kama vile Al-Tabari, Al-Zamakhshari na Al-Baydawi wanaiongezea hadithi. Hapa wanadai kwamba jina Malkia ni Bilkīs ( (Kiar. بلقيس)[5] ), pengine limetokana na Kigiriki παλλακίς pallakis iliyomaanisha "suria". Qur'ani haitaji jina la Malkia, inasema tu "mwanamke anayewatawala" ( Kiar. امْرَأَةً تَمْلِكُهُمْ ) [17] watu wa Sheba.
Marejeo
hariri- ↑ E. Ullendorff (1991), "BILḲĪS", The Encyclopaedia of Islam, juz. la 2 (tol. la 2nd), Brill, ku. 1219–1220
- ↑ National Geographic, issue mysteries of history, September 2018, p.45.
- ↑ Samuel Abramsky; S. David Sperling; Aaron Rothkoff; Haïm Zʾew Hirschberg; Bathja Bayer (2007), "SOLOMON", Encyclopaedia Judaica, juz. la 18 (tol. la 2nd), Gale, ku. 755–763
- ↑ Yosef Tobi (2007), "QUEEN OF SHEBA", Encyclopaedia Judaica, juz. la 16 (tol. la 2nd), Gale, uk. 765
- ↑ 5.0 5.1 5.2 E. Ullendorff (1991), "BILḲĪS", The Encyclopaedia of Islam, juz. la 2 (tol. la 2nd), Brill, ku. 1219–1220
- ↑ Samuel Abramsky; S. David Sperling; Aaron Rothkoff; Haïm Zʾew Hirschberg; Bathja Bayer (2007), "SOLOMON", Encyclopaedia Judaica, juz. la 18 (tol. la 2nd), Gale, ku. 755–763
- ↑ Yosef Tobi (2007), "QUEEN OF SHEBA", Encyclopaedia Judaica, juz. la 16 (tol. la 2nd), Gale, uk. 765
- ↑ E. Ullendorff (1991), "BILḲĪS", The Encyclopaedia of Islam, juz. la 2 (tol. la 2nd), Brill, ku. 1219–1220
- ↑ Samuel Abramsky; S. David Sperling; Aaron Rothkoff; Haïm Zʾew Hirschberg; Bathja Bayer (2007), "SOLOMON", Encyclopaedia Judaica, juz. la 18 (tol. la 2nd), Gale, ku. 755–763
- ↑ Yosef Tobi (2007), "QUEEN OF SHEBA", Encyclopaedia Judaica, juz. la 16 (tol. la 2nd), Gale, uk. 765
- ↑ Belcher, Wendy Laura (2010-01-01). "From Sheba They Come: Medieval Ethiopian Myth, US Newspapers, and a Modern American Narrative". Callaloo. 33 (1): 239–257. doi:10.1353/cal.0.0607. JSTOR 40732813. S2CID 161432588.
- ↑ Munro-Hay, Stuart (2006-10-31). The Quest for the Ark of the Covenant: The True History of the Tablets of Moses (kwa Kiingereza) (tol. la New). I.B.Tauris. ISBN 9781845112486.
- ↑ Munro-Hay, Stuart (2004). "Abu al-Faraj and Abu al-ʽIzz". Annales d'Ethiopie. 20 (1): 23–28. doi:10.3406/ethio.2004.1067.
- ↑ Ingawa hali halisi nasaba hiyo ilianzishwa tu katika karne ya 12 BK
- ↑ Littmann, Enno (1909), "Geschichte der äthiopischen Litteratur", katika Carl Brockelmann; Franz Nikolaus Finck; Johannes Leipoldt; Enno Littmann (whr.), Geschichte der christlichen Litteraturen des Orients (tol. la 2nd), Amelang, ku. 246–249
- ↑ https://www.clearquran.com/027.html
- ↑ Surat an-Naml 27:23
Kujisomea
hariri- Thaʿlabī, Qiṣaṣ ̣(1356 A.H.), 262–4
- Kisāʾī, Qiṣaṣ (1356 A.H.), 285–92
- G. Weil, The Bible, the Koran, and the Talmud ... (1846)
- G. Rosch, Die Königin von Saba als Königin Bilqis (Jahrb. f. Prot. Theol., 1880) 524‒72
- M. Grünbaum, Neue Beiträge zur semitischen Sagenkunde (1893) 211‒21
- E. Littmann, The legend of the Queen of Sheba in the tradition of Axum (1904)
- L. Ginzberg, Legends of the Jews, 3 (1911), 411; 4 (1913), 143–9; (1928), 288–91
- H. Speyer, Die biblischen Erzählungen im Qoran (1931, repr. 1961), 390–9
- E. Budge, The Queen of Sheba and her only son Menyelek (1932)
- J. Ryckmans, L'Institution monarchique en Arabie méridionale avant l'Islam (1951)
- E. Ullendorff, Candace (Acts VIII, 27) and the Queen of Sheba (New Testament Studies, 1955, 53‒6)
- E. Ullendorff, Hebraic-Jewish elements in Abyssinian (monophysite) Christianity (JSS, 1956, 216‒56)
- D. Hubbard, The literary sources of the Kebra Nagast (St. Andrews University Ph. D. thesis, 1956, 278‒308)
- La Persécution des chrétiens himyarites au sixième siècle (1956)
- Bulletin of American Schools of Oriental Research 143 (1956) 6–10; 145 (1957) 25–30; 151 (1958) 9–16
- A. Jamme, La Paléographique sud-arabe de J. Pirenne (1957)
- R. Bowen, F. Albright (eds.), Archaeological Discoveries in South Arabia (1958)
- Encyclopedic Dictionary of the Bible (1963) 2067–70
- T. Tamrat, Church and State in Ethiopia (1972) 1270–1527
- W. Daum (ed.), Die Königin von Saba: Kunst, Legende und Archäologie zwischen Morgenland und Abendland (1988)
- J. Lassner, Demonizing the Queen of Sheba: Boundaries of Gender and Culture in Postbiblical Judaism and Medieval Islam (1993)
- M. Brooks (ed.), Kebra Nagast (The Glory of Kings) (1998)
- J. Breton, Arabia Felix from the Time of the Queen of Sheba: Eighth Century B.C. to First Century A.D. (1999)
- D. Crummey, Land and Society in the Christian Kingdom of Ethiopia: From the Thirteenth to the Twentieth Century (2000)
- A. Gunther (ed.), Caravan Kingdoms: Yemen and the Ancient Incense Trade (2005)
Viungo vya Nje
hariri- media kuhusu Queen of Sheba pa Wikimedia Commons
- BBC history of Queen Sheba
- More information on Queen Sheba Archived 5 Agosti 2005 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Malkia wa Sheba kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |