[[Picha:|300px|thumb|Malouma jukwaani mwaka 2004]] Malouma Mint El Meidah (kwa Kiarabu: المعلومة منت الميداح, pia Maalouma au Malouma; * 1 Oktoba 1960) ni mwimbaji, mtunzi wa nyimbo na mwanasiasa nchini Mauritania. Kisha kuzaliwa katika familia ya waimbaji, alipokuwa na miaka 12 alishiriki mara ya kwanza katika tamasha ya uimbaji. Baada ya kipindi cha kupumzika uimbaji wake kutokana na kuolewa na mume aliyemkataa alirudi kwenye jukwaa.

Malouma

Amezaliwa
Mauritania
Nchi Mauritania
Kazi yake Msanii na Mwanasiasa

Tangu miaka ya 1990 aliingia katika siasa akipigania demokrasia. Tangu mwaka 2007 amechaguliwa na kurudishwa kama mbunge wa senati.

Ametunga nyimbo nyingi pamoja na muziki na kushiriki kwenye tamasha za kimataifa.

Familia

hariri

Alizaliwa 1 Oktoba 1960 katika mji mdogo wa Mederdra katika Mauritania kusini magharibi. Familia yake ilikuwa ya waimbaji na wanamuziki, hivyo alifundishwa tangu utotoni kuimba na kutumia ala za muziki. Pamoja na kusikiliza muziki wa kimapokeo wa Kiberber, alipenda pia uimbaji wa Kiarabu kama nyimbo za Umm Kalthoum au Fairuz. Alipokua alianza kuvutwa pia na muziki wa blues.

Uimbaji

hariri

Aliandika wimbo wa kwanza alipokuwa na umri wa miaka 16 "Habibi Habeytou" (Mpenzi wangu, nilimpenda). Humo alikosolea kawaida ya wanaume kuwafukuza wake katika nyumba wakipata mke mpya kijana. Wimbo huu ulimletea umaarufu lakini alishambuliwa pia na wengine. Baadaye alihamia pamoja na familia yake kwenye mji mkuu Nouakchott ili apate nafasi pana zaidi kwa muziki wake.

Lakini katika mazingira ya kuongozwa na mapokeo aliolewa na kuacha tamasha hadi mwisho wa miaka ya 1980.

Mwaka 1988 aliimba kwenye tamasha ya Karthago huko Tunis. Katiba nyimbo zake aligusa masuala kama umaskini, magonjwa, na uhuru wa maoni. Kuanzia hapo alionyeshwa pia kwenye vituo vya runinga vya nchi za Kiarabu. Nyumbani kwake alikataliwa sasa kuwa na tamasha au nyimbo zake kurushwa kwenye runinga au redio.[1]

Wakati huo Malouma alianza kushiriki katika siasa akajiunga na chama cha upinzani kilichodai mwisho wa udikteta. Baada ya kukataliwa kwenye media za Mauretania pia albamu yake ya kimataifa ilipigwa marufuku mwaka 1998, lakini vijana walimpenda.

Hatimaye mwaka 2003 kulitokea maandamano ya wananchi 10,000 mjini Nouakchott waliodai uhuru kwa uimbaji wake na rais Ould Taya alimkubali.[2]

 
Tamasha mwaka 2012 kwenye ubalozi wa Marekani, Nouakchott

Mwaka 2007 Mauretania iliona uchaguzi huru wa kwanza wa historia yake na Malouma alichaguliwa kuwa mbunge wa senati akiwa mmoja wa wanawake sita kati ya maseneta 56[3]. Serikali mpya ilipopinduliwa na wanajeshi mwaka 2008, Malouma alitunga nyimbo za kupinga uasi huu akakamatwa. Katika uchaguzi uliofuata akarudishwa kwenye senati upande wa upinzani.

Mwaka 2014 Malouma aliachana na upinzani akahamia upande wa chama cha serikali.

Marejeo

hariri
  1. All about Maalouma Archived 30 Januari 2016 at the Wayback Machine., Malouma and the Sahel Hawl Blues, Teacher resource guide, University Musical Society, University of Michigan, Ann Arbour 04/05
  2. Malouma, la chanteuse du peuple Archived 23 Septemba 2017 at the Wayback Machine. UMS University of Michigan Musical Society, Teacher Resource Guide, 04/05
  3. "المعلومة بنت الميداح.. ألحان الفن وأحلام السياسة". Al Jazeera (in Arabic). Doha, Qatar: Al Jazeera Encyclopedia. 12 February 2014. Retrieved 16 January 2016.

Viungo vya Nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: