Maria Maajabu wa Yesu
Maria Maajabu wa Yesu, O.C.D. (jina la awali kwa Kihispania: Maravillas Pidal y Chico de Guzmán; Madrid, Hispania, 4 Novemba 1891 - La Aldehuela, 11 Desemba 1974) alikuwa mwanamke mmonaki wa shirika la Wakarmeli Peku aliyeanzisha monasteri nyingi hadi India, akiunganisha maisha ya sala na upendo wa matendo [1].
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 10 Mei 1998 akamtangaza mtakatifu bikira tarehe 4 Mei 2003.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 11 Desemba[2].
Tazama pia
haririMarejeo
haririViungo vya nje
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |