Maria Mikaela Desmaisieres

Maria Mikaela Desmaisieres (Madrid, Hispania, 1 Januari 1809Valencia, 24 Agosti 1865) alikuwa mtawa aliyeanzisha shirika la Masista Waabuduo Wajakazi wa Sakramenti Kuu na wa Upendo.

Mt. Maria Mikaela.

Kabla ya hapo aliacha maisha ya fahari ya familia yake akahudumia waliopatwa na kipindupindu na makahaba[1].

Hatimaye alihudumia tena wenye kipindupindu nayo ikampata na kumuua.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu. Alitangazwa na Papa Pius XI kuwa mwenye heri tarehe 7 Juni 1925, halafu mtakatifu tarehe 4 Machi 1934.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 24 Agosti[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.