Maria Yosefa Rossello
Maria Giuseppa Rossello, FdM (27 Mei 1811 – 7 Desemba 1880) alikuwa mtawa wa Italia aliyeanzisha shirika la Mabinti wa Bibi Yetu wa Huruma, lenye lengo la kueneza huruma ya Mungu ulimwenguni, akajitoa kwa ari kuokoa watu kiroho, akimtegemea Mungu tu [1].
Alitangazwa na Papa Pius XI kuwa mwenye heri tarehe 6 Novemba 1938, halafu na Papa Pius XII kuwa mtakatifu tarehe 12 Juni 1949.[2]
Maisha
haririBenedetta Rossello alizaliwa Albissola Marina akiwa mtoto wa 4 kati ya 10.
Alisaidia wazazi wake, Bartolomeo Rossello na Maria Dedone, katika shughuli za nyumbani na malezi ya wadogo wake.
Alikuwa na heshima kwa Bikira Maria na kunuia kufuata wito wake wa kitawa. Hivyo alijiunga na Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko alipokuwa na umri wa miaka 16.
Baada ya misiba mbalimbali, Benedetta alibaki tegemeo la familia yote.[4]
Mwaka 1837 Rosello aliitikia wito wa Agostino De Mari wa kujitolea kulea watoto maskini akapatiwa nyumba ndogo kwa ajili yake na ya wasaidizi wake. Ndiyo chanzo cha shirika tarehe 10 Agosti 1837. Mara akawa mlezi na mhasibu wake.
Tarehe 22 Oktoba 1837 walianza unovisi rasmi akapewa jina la Maria Giuseppa.
Shirika jipya lilifanya kazi kati ya mafukara na wagonjwa, likisaidia katika parokia, hospitali na shule.[5]
Mwaka 1840 Rossello akawa mkuu wa shirika kwa miaka 40.
Kutokana na uchovu, alipatwa na matatizo ya moyo, akafariki akiwa na miaka 69 tarehe 7 Desemba 1880.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/35600
- ↑ St. Maria Giuseppa Rossello. Catholic Online. Retrieved on 3 May 2015.
- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ Saint Mary Joseph Rossello. Roman Catholic Saints. Retrieved on 3 May 2015.
- ↑ St. Maria Giuseppa Rossello. Catholic Online. Retrieved on 3 May 2015.