Huruma ya Mungu ni sifa kubwa ya Mwenyezi Mungu ambayo inatangazwa katika dini mbalimbali, hususan Uyahudi, Ukristo na Uislamu.

Picha ya Huruma ya Mungu ilivyochorwa na Eugeniusz Kazimirowski, 1934.
Sanamu ya Huruma ya Mungu, Coronel Fabriciano,Brazil.

Biblia na Kurani zinalingana katika kusisitiza ubora wa sifa hiyo.

Katika Kanisa Katoliki

hariri

Ibada kwa sifa hiyo imepata msukumo wa pekee katika Kanisa Katoliki katika karne ya 20 kutokana na ufunuo wa binafsi aliopewa sista Faustina Kowalska mwaka 1935.

Baada ya kushinda shaka na upinzani, ibada hiyo ilieneza kwa nguvu na Papa Yohane Paulo II ambaye mwaka 2000 alimtangaza sista huyo kuwa mtakatifu na kutekeleza utabiri wake wa kwamba siku moja Sikukuu ya Huruma ya Mungu itaadhimishwa na Papa siku ya nane (Oktava) ya Pasaka.

Kabla ya hapo Papa huyo alikuwa ametoa Enciclica yake ya pili juu ya huruma hiyo (Dives in Misericordia, 1980).

Picha ya Yesu mwenye huruma

hariri

Picha hiyo inamchora Yesu mwenye huruma kufuatana na maelezo ya sista Faustina kuhusu njozi alizopata.

Yesu anaonekana ameinua mkono wa kulia huku miali miwili ikimtoka moyoni, mmojawapo ukiwa mweupe na mwingine mwekundu, ikiwakilisha maji na damu vilivyomtoka ubavuni baada ya kuchomwa na askari kwa mkuki ili kuhakikisha kifo chake.

Yesu amechorwa akiwa na kanzu nyeupe yenye kung'aa mbele ya rangi ya buluu. Chini kuna maneno ya Kipolandi, "Jezu, ufam tobie" ("Yesu, nakutumainia").

Rosari ya Huruma ya Mungu

hariri

Sala ya kilitania kwa Huruma ya Mungu inafanyika kwa kutumia rosari ya kawaida, ila maneno yanayokaririwa ni tofauti.


  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.