Martino wa Braga (Panonia, leo Hungaria, 510 hivi - Braga, Ureno, 20 Machi 579) alikuwa mmonaki huko Palestina[1], halafu alihamia sehemu iliyotazamwa kama mwisho wa dunia, akawa mmisionari kati ya Waswevi walioteka Hispania kaskazini mashariki[2]. Baada ya kuanzisha monasteri mbalimbali, akawa askofu wa Dumio na hatimaye askofu mkuu wa Braga[3].

Mchoro mdogo wa Mt. Martino.

Msomi mkubwa sana[4], aliacha maandishi mbalimbali. Hasa kwa juhudi zake alifaulu kuwafanya watu wa kabila hilo la Wagermanik waache Uario na kujiunga na Kanisa Katoliki.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu[5].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 20 Machi[6].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Ott, Michael. "St. Martin of Braga." The Catholic Encyclopedia. Vol. 9. New York: Robert Appleton Company, 1910. 12 Mar. 2013
  2. Collins, Early Medieval Spain: Unity in Diversity 400-1000, second edition (New York: St. Martins, 1995), p. 81
  3. M.L.W. Laistner, Thought and Letters in Western Europe: A.D. 500 to 900, second edition (Ithaca: Cornell University, 1957), p. 117
  4. Decem Libri Historiarum, V.37; translated by Lewis Thorpe, History of the Franks (Harmondsworth: Penguin, 1974), p. 301
  5. http://www.santiebeati.it/dettaglio/91426
  6. Martyrologium Romanum

Marejeo hariri

  • M.L.W. Laistner, Thought and Letters in Western Europe: A.D. 500 to 900, second edition (Ithaca: Cornell University, 1957), p. 117.
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.