Maximilian Kolbe
Maximilian Maria Kolbe (8 Januari 1894 – 14 Agosti 1941) alikuwa padre wa Kanisa Katoliki na mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo Wakonventuali kutoka nchi ya Poland.
Katika historia ya Kanisa anajulikana kwa jinsi allivyomheshimu Bikira Maria kwa jina la Imakulata, yaani Mkingiwa dhambi ya asili.
Baada ya kuanzisha chama cha Mashujaa wa Imakulata huko Roma (Italia) na Mji wa Imakulata huko Polandi, alikwenda Japani kama mmisionari.
Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia alifungwa na wafuasi wa Unazi sehemu mbalimbali na hatimaye katika kambi ya wafungwa wa siasa kule Auschwitz. Huko alijitoa kafara ya upendo na uaminifu kwa Mungu na binadamu kwa kushika nafasi ya mfungwa mwenzake aliyechaguliwa kuachwa bila chakula hadi kufa pamoja na wengine 9. Aliwaandaa hao wote kukabili kifo kwa tumaini la Kikristo na bila ya chuki, na alipobaki peke yake aliuawa kwa sindano ya sumu[1].
Papa Paulo VI alimtangaza mwenye heri tarehe 17 Oktoba 1971, halafu Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu mfiadini tarehe 10 Oktoba 1982.
Sala yake
haririWewe umenipenda milele, tangu u Mungu; hivyo umenipenda na utanipenda milele!...
Upendo wako kwangu ulikuwepo hata kabla sijakuwepo, na ni kwa sababu ya kunipenda, Mungu mwema, kwamba umeniita kutoka utovu wa vyote nianze kuwepo!
Tazama pia
haririTanbihi
haririMarejeo
hariri- B. HANLEY, O.F.M., Maximilian Kolbe, Upendo uliokithiri – tafsiri ya Parokia la Mt. Maksimilian Kolbe, Mwenge, Dar-es-Salaam – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1992
- Rees, Laurence. Auschwitz: A New History, Public Affairs, 2005. ISBN 1-58648-357-9
Viungo vya nje
hariri- Patron Saints Index: Saint Maximilian Kolbe Ilihifadhiwa 16 Aprili 2008 kwenye Wayback Machine.
- Kolbe's Gift, a play by David Gooderson about Kolbe and his self-sacrifice in Auschwitz based on factual evidence and conversations with the late Józef Garliński
- Saint Maximilian Kolbe, a popular biography at Catholicism.org
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |