Mfalme Hezekia
Mfalme Hezekia (kwa Kiebrania: יְחִזְקִיָּ֫הוּ, H̱izkiyyahu, H̱izkiyya, Yeẖizkiyyahu, Ḥizqiyyā́hû, Ḥizqiyyā, Yəḥizqiyyā́hû, Hizqiyyahu ben Ahaz; kwa Kigiriki: Ἐζεκίας, Ezekias) alitawala ufalme wa Yuda kati ya miaka 729 KK na 716 KK pamoja na baba yake mfalme Ahazi, halafu peke yake hadi mwaka 697 KK, tena pamoja na mwanae Manase hadi kifo chake mwaka 687 KK.
Ni mmojawapo kati ya wafalme wachache wanaosifiwa na Biblia kuwa alifanana na mfalme Daudi, babu yake, kwa kuwa alijitahidi kufanya urekebisho wa kidini ili raia zake wamuabudu YHWH tu.
Habari zake zinapatikana hasa katika Kitabu cha Pili cha Wafalme 18-20, Isaya 36-39 na Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati 29-32, mbali ya kitabu cha Methali 25:1.
Pia anatajwa katika vitabu vya manabii Yeremia, Amosi na Hosea.
Hatimaye anatajwa na Injili ya Mathayo kati ya mababu wa Yesu Kristo.
Anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Agosti.
Tazama pia
haririTanbihi
haririMarejeo
hariri- Grena, G.M. (2004). LMLK—A Mystery Belonging to the King vol. 1. Redondo Beach, California: 4000 Years of Writing History. ISBN 0-9748786-0-X.
- Austin, Lynn. Gods And Kings. ISBN 0-7642-2989-3. a fictionalized account of Hezekiah's rise to power, Book 1 in Austin's "Chronicles of the Kings" series
Viungo vya nje
hariri- "Hezekiah." Encyclopædia Britannica. Encyclopædia Britannica Online.
- King Hezekiah Archived 24 Oktoba 2005 at the Wayback Machine. from Jerusalem Mosaic
- Hezekiah Archived 8 Desemba 2010 at the Wayback Machine. See all Bible verses pertaining to King Hezekiah
- The Reign Of Hezekiah Archived 23 Julai 2009 at the Wayback Machine. by John F. Brug
- "Ezechias". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.
- Sennacherib's Invasion of Hezekiah's Judah in 701 BC - by Craig C. Broyles
- Interactive Map of Sennacherib's Invasion of Hezekiah's Judah, including the accounts of Sennacherib, Herodotus, 2 Kings, Isaiah and Micah Archived 13 Machi 2009 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mfalme Hezekia kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |