Mgongo kati wa bahari
Mgongo kati wa bahari (kwa Kiingereza: Mid-oceanic ridge, kifupi: MOR) ni safu ya milima ya kivolkeno kwenye sakafu ya bahari, mita elfu kadhaa chini ya uso wake. Milima hii inapatikana kwenye mpaka wa mabamba mawili ya gandunia yanayoachana na hivyo kuacha ufa ambako magma moto kutoka chini inapanda juu.
Kutokea kwa milima ya kivolkeno chini ya bahari
haririWakati wa kutoka na kuingia katika maji, magma iliyo katika hali ya kiowevu huganda na kujenga safu ndefu ya milima ya kivolkeno. Katikati, kwenye kilele cha safu, mara nyingi kuna ufa kama mfereji ambako magma inazidi kupanda juu inapoanza kuganda na kuwa mwamba thabiti pande zote mbili za mfereji.
Kwa hiyo kwenye mistari ya migongo kati ya bahari hutokea mfululizo ganda jipya la Dunia. Mchakato huo huitwa upanuzi wa sakafu ya bahari (ing. seafloor spreading).
Migongo ya bahari inapatikana katika kila bahari kubwa. Sehemu kubwa zaidi katika mfumo huo ni Mgongo kati wa Atlantiki ambako Bahari Atlantiki inapanuka sentimita mbili kila mwaka.
Visiwa
haririKatika sehemu kadhaa volkeno zinazoanza kwenye sakafu ya bahari zinazidi kukua hadi kupotoka kwenye uso wa maji na kuunda visiwa baharini. Mifano ni pamoja na visiwa vya Azori na kisiwa cha Ascension katika Atlantiki.
Mfano maalumu usio kawaida ni kisiwa cha Iceland kilichoanza hivihivi lakini ni kikubwa kulingana na visiwa vingine vya aina hii. Huko sehemu ya mgongo kati wa Atlantiki imeinuliwa juu pamoja na ufa ambako magma iliyotoka nje wakati ulikuwepo bado chini ya bahari. [1]
Topografia
haririPale ambapo ufa kati ya mabamba gandunia na hivyo mgongo wa bahari zinatokea, bahari huwa mara nyingi na kina cha mita 2,600 hivi [2]
Hali halisi safu hizi za kivolkeno mara nyingi hazipo katikati ya beseni la bahari, kwa mfano kwenye Pasifiki ziko upande, karibu na pwani ya Amerika. Lakini safu iliyotambuliwa mapema ilikuwa Mgongo kati wa Atlantiki iliyounda lugha ya "mid-ocean ridge" yaani mgongo kati wa bahari na jina hili linaendelea kutumiwa hata kama siku hizi zinaitwa pia "oceanic ridges" pekee.[3]
Tabia za migongo hiyo hutofautiana kulingana na kasi ya kupanuka.
Kasi ya kupanuka kwa mgongo imepimwa kati ya milimita 10 hadi 200.[4] Mgongo unaopanuka polepole kama ule wa Atlantiki huwa juu zaidi na kuonyesha mtelemko mkali kuliko mgongo unaopanuka haraka kama ule wa Pasifiki ya Mashariki wenye mitelemko midogo.
Mgongo unaopanuka polepole (chini ya mm 40 kwa mwaka) mara nyingi huwa na bonde la ufa kubwa katikati lililokadiriwa kuwa na upana hadi km 10 – 20 na vilele vikali. [5] [6]
Kinyume chake, mgongo unaopanuka haraka (zaidi ya mm 90/mwaka) kama ule kwenye Pasifiki Mashariki hukosa bonde la ufa.[7]
Tanbihi
hariri- ↑ Trond H. Torsvik, Hans E. F. Amundsen, Reidar G. Trønnes, Pavel V. Doubrovine, Carmen Gaina, Nick J. Kusznir, Bernhard Steinberger, Fernando Corfu, Lewis D. Ashwal, William L. Griffin, Stephanie C. Werner, Bjørn Jamtveit: Continental crust beneath southeast Iceland. Proceedings of the National Academy of Science of the United States of America. Bd. 112, Nr. 15, 2015, E1818–E1827, doi:10.1073/pnas.1423099112
- ↑ Macdonald, Ken C. (2019), "Mid-Ocean Ridge Tectonics, Volcanism, and Geomorphology", Encyclopedia of Ocean Sciences (kwa Kiingereza), Elsevier, ku. 405–419, doi:10.1016/b978-0-12-409548-9.11065-6, ISBN 9780128130827, iliwekwa mnamo 2019-06-20
- ↑ Oceanic ridge system, tovuti ya Britannica, iliangaliwa Novemba 2019
- ↑ Searle, Roger, 1944: Mid-ocean ridges isbn 9781107017528
- ↑ Macdonald, Ken C. (1977). "Near-bottom magnetic anomalies, asymmetric spreading, oblique spreading, and tectonics of the Mid-Atlantic Ridge near lat 37°N". Geological Society of America Bulletin (kwa Kiingereza). 88 (4): 541. Bibcode:1977GSAB...88..541M. doi:10.1130/0016-7606(1977)88<541:NMAASO>2.0.CO;2. ISSN 0016-7606.
- ↑ Macdonald, K. C. (1982). "Mid-Ocean Ridges: Fine Scale Tectonic, Volcanic and Hydrothermal Processes Within the Plate Boundary Zone". Annual Review of Earth and Planetary Sciences. 10 (1): 155–190. Bibcode:1982AREPS..10..155M. doi:10.1146/annurev.ea.10.050182.001103.
- ↑ Argus, Donald F.; Gordon, Richard G.; DeMets, Charles (2010-04-01). "Geologically current plate motions". Geophysical Journal International (kwa Kiingereza). 181 (1): 1–80. Bibcode:2010GeoJI.181....1D. doi:10.1111/j.1365-246X.2009.04491.x. ISSN 0956-540X.
Marejeo
hariri- Roger Searle: Mizunguko wa Mid-Ocean. Vyombo vya Habari vya Chuo Kikuu cha Cambridge. Cambridge (UK) 2013, ISBN 978-1-107-01752-8
- Wolfgang Frisch, Martin Meschede: Viungo vya Plate. Mabadiliko ya Bara na malezi ya mlima. 5, toleo lililosasishwa. Primus Verlag, Darmstadt 2013, ISBN 978-3-86312-366-6