Mikaeli wa Watakatifu

Mikaeli wa Watakatifu (jina la awali: Miquel Argemir; Vic[1], Catalonia, Hispania, 29 Septemba 1591 - Valladolid, Hispania, 10 Aprili 1625) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mtawa wa shirika la Watrinitari, yaani watawa wa Utatu mtakatifu, waliojitoa kabisa kwa ajili ya kukomboa Wakristo waliotekwa utumwani.

Sanamu yake.

Alijiunga na urekebisho wa shirika hilo lililofanywa na Yohane Mbatizaji Garcia kwa kuanzisha tawi la Watrinitari Peku kwa kufuata mfano wa Teresa wa Yesu.

Alijitosa kuhudumia watu kwa matendo ya huruma na kuhubiri Neno la Mungu.

Pia aliandika vitabu vichache juu ya maisha ya kiroho zake za pekeekufuatana na mang'amuzi na karama [2].

Alitangazwa na Papa Pius VII kuwa mwenyeheri tarehe 26 Septemba 1819, halafu Papa Paulo VI alimtangaza mtakatifu tarehe 25 Mei 1975[3].

Sikukuu yake ni tarehe 10 Aprili[4].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. About the Trinitarian Saints and Blesseds. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-02-03. Iliwekwa mnamo 2021-04-02.
  2. http://www.santiebeati.it/dettaglio/91533
  3. Saint John Baptist of the Conception. Santi e Beati.
  4. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.