Milenia ya 6 KK
milenia
Lango la Historia | Lango la Biografia | Karibuni | Orodha ya Miaka
◄ | Milenia ya 7 KK | Milenia ya 6 KK | Milenia ya 5 KK | ►
Makala hii inahusu milenia ya 6 KK (miaka 5999 KK - 5000 KK). Katika sehemu nyingi za dunia tunaona mwanzo wa kilimo.
Matukio
hariri- Kisiwa cha Britania (Uingereza na Uskoti) hutenganishwa kutoka kwa Ulaya bara kwa kupanda ya uwiano wa bahari. Sababu yake ni badiliko la halijoto linalosababisha kuyeyuka kwa barafuto nchini na barafu yake kuwa maji mengi yanayopandisha uwiano wa bahari.
- Mnamo 5800 KK kunatokea banguko kubwa chini ya bahari kwenye tako la bara karibu na pwani ya Norwei (banguko la Storegga). Banguko hilo lilisababisha tsunami iliyoharibu vijiji vya watu huko Uskoti.
- katika eneo la Mediteranea hali ya hewa ni ya kitropiki
- Misri kuna kilimo kwenye bonde la Naili
- plau inavumbuliwa
- tangu 6000 KK: kuku wanaanza kufugwa nchini China
- tangu 6000 KK: mizabibu ya kwanza inapandwa katika Kaukazi na Mesopotamia.
- tangu 5600 KK: kilimo kinaanza Ulaya ya Kati
- tangu 5600 KK: Eneo la Sahara linazidi kuwa kabisi na kuwa jangwa; watu huondoka.
- mnamo 5500 KK: umwagiliaji wa mashamba katika Mesopotamia
- mnamo 5500 KK: vifaa vilivyofinyangwa vya kwanza katika Asia kusini
- baina ya 5500 na 5300 KK: mtama unaanza kulimwa huku China Kaskazini
- mnamo 5200 KK: mahekalu ya kwanza katika Mesopotamia
- mnamo 5100 KK: mahindi, maharagwe, mboga na maparachichi hupandwa katika Amerika ya Kati
- mnamo 5000 KK: mpunga hulimwa kwenye pwani ya China
Watu
haririTanbihi
hariri
Viungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Milenia ya 6 KK kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |