Mitrofani Chi Sung
Mitrofani Chi Sung (Cháng Yángjí,常楊吉; 10 Desemba 1855 – 10 Juni 1900) alikuwa padri wa kwanza wa Kanisa la Kiorthodoksi la China kufia dini ya Ukristo.
Alikuwa amekubali kwa shida kupewa upadrisho huko Tokyo, Japani mwaka 1880, akijiona hana sifa.
Ndiye maarufu zaidi kati ya wafiadini wa China 222 wa Kanisa hilo waliotangazwa watakatifu mwaka 2000[1], wakiwemo watu wa familia yake (mke Tatiana Li na watoto Isaya na Yohane).