Moyo Safi wa Maria

(Elekezwa kutoka Moyo safi wa Maria)

Moyo Safi wa Maria ni namna Wakatoliki wanavyomheshimu Bikira Maria kwa maisha yake ya Kiroho kama yanavyodokezwa na Luka katika Injili yake. Humo alisisitiza tabia ya Mama wa Yesu ya kuweka na kutafakari moyoni mwake yote yaliyomhusu Mwanae.[1][2]

Logo ya Moyo Safi.

Kwa kawaida moyo wake unachorwa umechomwa kwa panga saba au una vidonda saba kulingana na mateso yaliyompata kwa ajili ya Yesu.

Heshima kwa moyo wa Maria inaendana na ibada kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu[3].

Kati ya watakatifu waliowahi kuwa na heshima hiyo kuna Anselm wa Canterbury, Bernardo wa Clairvaux, Matilda wa Ringelheim, Gertrudi wa Thuringia na Brigita wa Uswidi.[4]

Baadaye Yohane Eudes (alifariki 1681) alieneza heshima hiyo na kufanya iwe na adhimisho katika kalenda ya liturujia, kwanza huko Autun mwaka 1648 halafu katika majimbo mengine ya Ufaransa. Pia alianzisha mashirika mbalimbali kwa ajili hiyo na kutoa kitabu kikubwa Coeur Admirable (Moyo wa Ajabu, 1681).[5][6]

Hatimaye, mwaka 1805 Papa Pius VII aliruhusu sikukuu ya namna hiyo.[7]

Tanbihi

hariri
  1. "Mauriello, Rev. Matthew R., "Devotion to the Immaculate Heart of Mary", University of Dayton". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Julai 2013. Iliwekwa mnamo 29 Juni 2013. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Bainvel, Jean. "Devotion to the Immaculate Heart of Mary". The Catholic Encyclopedia. Vol. 7. New York: Robert Appleton Company, 1910. 20 December 2012
  3. "The Immaculate Heart of Mary", Catholic News Agency
  4. Roten, Johan G. "The Heart of Mary", Marian Library, University of Dayton, June 4, 2013
  5. "EWTN on the Hearts of Jesus and Mary". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-05-12. Iliwekwa mnamo 2020-06-19.
  6. Life of the Venerable John Eudes by Charles De Montzey, Cousens Press 2008, ISBN 1-4097-0537-4 page 215
  7. Saints and feasts of the liturgical year by Joseph N. Tylenda 2003 ISBN 0-87840-399-X page 118

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Moyo Safi wa Maria kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.