München

(Elekezwa kutoka Munchen)

München (kwa Kibavaria: Minga; kufuatana na uzoefu wa lugha ya Kiingereza Munich; tamka: Munik) ni mji mkubwa wa tatu nchini Ujerumani (baada ya Berlin na Hamburg) na mji mkuu wa jimbo la Bavaria lililopo kusini mwa Ujerumani.

Kanisa kuu na jumba la manispaa ya München
Nguzo ya Bikira Maria.

Uko kando ya mto Isar takriban mita 500 juu ya UB.

Milima ya Alpi iko karibu.

Idadi ya wakazi ni 1,320,000, lakini rundiko la jiji lina wakazi milioni mbili na nusu.

München ni kati ya vitovu muhimu vya uchumi, utamaduni na sayansi vya Ujerumani.

Klabu ya soka ya Bayern München imeshinda mara 19 kombe la kitaifa na mara tatu kombe la Ulaya.

Historia

hariri

Jina la mji linatokana na makazi ya wamonaki waliokuwa na nyumba kando ya Isar yaliyotajwa mara ya kwanza katika hati ya mwaka 1158.

Mji ukawa soko kwenye daraja la kuvuka mto.

Baada ya kuwa makao makuu ya watawala wa Bavaria mji ulianza kukua. Mnamo mwaka 1700 ulikuwa na wakazi 24,000 pekee walioongezeka kuwa 170,000 mnamo 1871 na 840,000 mwaka 1933.

Tazama pia

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


  Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu München kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.