Muungano wa Kimataifa wa Mawasiliano

Muungano wa Kimataifa wa Mawasiliano (kwa Kiingereza: International Telecommunication Union; kifupi: ITU) ni wakala maalum wa Umoja wa Mataifa anayewajibika kwa masuala yote yahusuyo teknolojia ya mawasiliano na habari (information and communications technology) [1] ambalo ni shirika kongwe ulimwenguni (international organization).

Muungano wa kimataifa wa mawasiliano
Muungano wa kimataifa wa mawasiliano

ITU inaratibu matumizi ya wigo wa radio wa pamoja (radio spectrum), inakuza ushirikiano wa kimataifa katika kupeana njia ama mzunguko wa satelaiti (orbit), inafanya kazi kukuza miundombinu ya mawasiliano ya ulimwengu unaoendelea, pia inasaidia katika maendeleo na uratibu wa viwango vya kiufundi vya kimataifa (technical standard). Umoja huu unahusika sana palipo mtandao wa intaneti, teknolojia za kisasa zisizo na waya, teknolojia ya anga na maji ya urambazaji, teknolojia ya unajimu, upatikanaji wa mtandao, matangazo ya televisheni, pamoja na teknolojia ya kisasa ya mtandao.

Historia

hariri

Maendeleo ya telegrafu mapema katika karne ya 19 yalibadilisha njia za mawasiliano baina ya watu kuanzia ngazi ya nchi mpaka kimataifa. Ongezeko la mawasiliano ya kimataifa lilipelekea uhitaji wa usanifu na ushirikiano kupita mipaka ya mataifa. Hii ni kwa sababu ya ukweli kuwa nyaya ilibidi zipitishwe kenye mipaka ya mataifa, jumbe ilibidi zizuiliwe ili ziweze kutafsiriwa kwenye mifumo mingine ya mamlaka.

Kati ya mwaka 1849 na 1865, mfululizo wa makubaliano baina ya nchi mbili ama kanda ulianzishwa kati ya majimbo ya Ulaya magharibi kwa ajili ya kujaribu kusanifu mawasiliano ya kimataifa. [2] Kufikia 1865 ilikubaliwa kuwa kuna uhitaji mkubwa wa makubaliano juu ya kubadilisha makubaliano yote ya zamani na kutengeneza mfumo wa usanikishaji vifaa vya telegrafu, kuweka sawa maelekezo ya uendeshaji pamoja na kuweka ushuru wa pamoja wa kimataifa na sheria za uhasibu. Kati ya tarehe 1 Machi na 17 Mei 1865, serikali ya Ufaransa ilikuwa mwenyeji wa wajumbe wa mataifa ishirini ya Ulaya katika Mkutano mkuu wa kwanza wa mawasiliano wa dunia uliofanyika mjini Paris. Makubaliano ya mkutano huo yalitiwa saini tarehe 17 Mei 1865. [2][3]

Marejeo

hariri
  1. International Telecommunication Union
  2. 2.0 2.1 "International Telegraph Conference (Paris, 1865)". International Telecommunication Union. International Telecommunication Union. n.d. Iliwekwa mnamo 1 Agosti 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Overview of ITU's History" (PDF). International Telecommunication Union. International Telecommunication Union. n.d. Iliwekwa mnamo 1 Agosti 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)