Nabii Yoeli
Nabii Yoeli (kwa Kiebrania יואל, Yoel, maana yake YHWH ni Mungu) alikuwa nabii wa Israeli ya Kale, labda katikati ya karne ya 4 KK.
Ujumbe wake unapatikana katika gombo la Manabii Wadogo la Biblia, kwa jina la Kitabu cha Yoeli. Humo tunasoma alivyotangazwa siku tukufu ya Bwana na fumbo la Roho Mtakatifu kumiminwa juu ya kila mtu, ambalo Wakristo wanaamini Mwenyezi Mungu alilitimiza kwa namna ya ajabu katika Yesu Kristo kwenye Pentekoste [1].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake kwa Wakatoliki na Waorthodoksi huwa tarehe 19 Oktoba[2][3] lakini awali pia tarehe 13 Julai.
Tazama pia
haririTanbihi
haririViungo vya nje
hariri- Four Prophets at Chabad.org
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nabii Yoeli kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |