Narsisi wa Yerusalemu

Narsisi wa Yerusalemu (99 - 216) alikuwa askofu wa 30 wa Yerusalemu, uliokuwa umejengwa upya kama mji wa Kipagani, kuanzia uzee mkubwa hadi kifo chake, ingawa katikati alikwenda kuishi upwekeni na nafasi yake ikashikwa na maaskofu wengine watatu[1].

Mt. Narsisi katika dirisha la kioo cha rangi.

Alisaidia kufanya Wakristo wa Palestina wakubali kuadhimisha Pasaka siku ya Jumapili kila mwaka, kwa kuwa ndiyo siku ya ufufuko wa Yesu.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 29 Oktoba[2] au 7 Agosti.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  • Rev. Hugo Hoever; S.O.Cist., whr. (1955). Lives of the Saints, For Every Day of the Year. New York: Catholic Book Publishing Co.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.