Papa Viktor I (au Victus I) alikuwa Papa kuanzia takriban 186/189 hadi kifodini chake takriban 197/201[1].

Papa Vikta I katika dirisha la kioo cha rangi (Semmering, Austria).

Alimfuata Papa Eleutero akafuatwa na Papa Zefirini.

Alikuwa Papa wa kwanza kutokea Afrika, labda Leptis Magna, leo nchini Libya.

Anajulikana hasa kwa msimamo wake mkali kuhusu suala la tarehe ya Pasaka, wakati kabla ya kufanywa Papa, tofauti kuhusu tarehe hiyo haikusababisha farakano.[2] Kwa kuwa alitenga na Kanisa walioadhimisha Pasaka ya Kikristo siku moja kabla ya Pasaka ya Kiyahudi, si Jumapili kama huko Roma, Ireneo na wengineo walimlaumu, kama alivyoandika Eusebi wa Kaisarea.

Hata hivyo, tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 28 Julai[3].

Tazama pia Edit

Maandishi yake Edit

Tanbihi Edit

Viungo vya nje Edit

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Viktor I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.