Ngong ni mji ulio karibu na Ngong Hills, sambamba na Bonde la Ufa, kusini magharibi kwa Nairobi, kusini mwa Kenya. Kuna vitongoji vya Nairobi kama Ongata Rongai, Kiserian, Matasia na Kitengela ambapo wakazi (ambao kimsingi ni wa Nairobi) hujenga nyumba katika maeneo ya utulivu mkubwa kuliko ya mji.

Ngong Hills, Kenya
Ngong, kusini magharibi kwa Nairobi, karibu na Bonde la Ufa (bofya ramani kulia)

Ngong ni kata ya kaunti ya Kajiado, Eneo bunge la Kajiado Kaskazini[1].

"Ngong" ni neno la Kimasai linalomaanisha "nguyu"[2] kutokana na vilele vinne vya ushi, ambayo inasimama peke yake kutoka eneo tambarare la Nairobi. Vilima vya Ngong, kutoka mteremko wa mashariki, vinaangalia Hifadhi ya Taifa ya Nairobi, na kaskazini mwa mji wa Nairobi. Vilima vya Ngong, kutoka mteremko wa magharibi, vinaangalia Bonde la Ufa futi 4000 chini, ambapo vijiji vya Wamaasai vimekuwa vikiendelezwa.

Idadi ya jumla ya wakazi wa Ngong ni 107,188 (sensa ya mwaka 2009[3]), na mwinuko wa Ngong ni mita 1961 katika urefu, lakini urefu wa milima ni kama mita 2460 juu ya usawa wa bahari. [4]

Katika miaka ya utawala wa ukoloni wa Uingereza, eneo kuzunguka vilima vya Ngong ilikuwa sehemu ya kilimo ya walowezi, nyumba nyingi za jadi za ukoloni bado zinaonekana katika eneo hilo.

Katika filamu ya 1985 Out of Africa, vilele vinne vya Ngong hutokea katika usuli kadhaa karibu na nyumba ya Karen Blixen's. Bado wakazi wa mitaa huripoti kuona simba katika vilima wakati wa miaka ya 1990.

Kaburi la wapweke la Denys Finch Hatton, iliyo na alama ya obelisk na bustani, iko kwenye mteremko wa mashariki wa vilima vya Ngong, inayoelekea hifadhi kubwa ya mbuga.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Electoral Commission of Kenya: Registered voters per polling station by electoral area/ward and constituency Archived Septemba 29, 2007, at the Wayback Machine
  2. ^ "FOUR DAYS - OLOGASAILE / MAGADI(BEAS 08)" (tour), Government of Kenya, 2006, BreakawayExpedition.com webpage: BreakawayExpedition-Tour.
  3. Sensa ya Kenya 2009 Archived 9 Januari 2019 at the Wayback Machine., tovuti ya KNBS, ilitazamwa Januari 2009.
  4. "Ngong, Kenya Page" (statistics), Falling Rain Genomics, Inc., 2004, FallingRain.com webpage: FallingRainCom-Ngong.

Viungo vya nje

hariri

Tanbihi

hariri