Orion (chombo cha angani)

(Elekezwa kutoka Orion (chombo cha anga-nje))

Orion ni chombo cha angani kinachotengenezwa na kampuni ya Lockheed Martin kwa ajili na NASA na ESA. Inakusudiwa kubeba hadi wanaanga sita mpaka Mwezi na hata sayari ya Mirihi. Kazi ya kuipanga ilianza mwaka 2005. Chombo cha Orion kitazinduliwa kwa roketi ya Space Launch System inayotarajiwa kupatikana mnamo mwaka 2021 [1].

Orion pamoja na kitengo cha huduma cha ESA (uchoraji)

Orion ambayo ni sehemu ya kubeba wanaanga inaunganishwa na kitengo cha huduma penye injini, tangi, betri na teknolojia ya kusafisha hewa (European Service Module) iliyopangwa na ESA na kutengenezwa na Airbus huko Ujerumani[2].

Safari zake zimepangwa kutoka kwenye kituo cha Kennedy Space Center huko Cape Canaveral, Florida, Marekani.

Kwa asili Orion ilipangwwa kwa mradi wa "Constellation" ya NASA iliyofutwa mnamo 2011. Katika mradi mpya Orion ilibaki lakini sasa inatarajiwa kurushwa kwa roketi mpya ya Space Launch System inayolenga kupeleka wanaanga hadi Mwezi na Mirihi hadi mwaka 2033. [3]

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. "Preliminary Report Regarding NASA's Space Launch System and Multi-Purpose Crew Vehicle" (PDF). NASA. Januari 2011. Iliwekwa mnamo Juni 18, 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Multi Purpose Crew Vehicle – European Service Module for NASA's Orion programme". , tovuti ya Airbus Defence and Space. Iliangaliwa Mei 2020
  3. "NASA Moon and Mars". nasa.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-07. Iliwekwa mnamo 2019-05-21.