Papa Sixtus III alikuwa Papa kuanzia tarehe 31 Julai 432 hadi kifo chake tarehe 19 Agosti 440[1]. Alitokea Roma, Italia.

Mtakatifu Sisto III.

Alimfuata Papa Selestini I akafuatwa na Papa Leo I.

Chini yake makanisa mbalimbali yalijengwa mjini Roma, hasa basilika la Bikira Maria lililowekwa wakfu kwa Mama wa Mungu kadiri ya sifa aliyopewa na Mtaguso wa Efeso (431). Pia alijitahidi kupatanisha maaskofu wa Mashariki (Aleksandria na Antiokia) na kutetea mamlaka ya Kanisa la Roma juu ya Iliriko[2].

Rafiki wa Agostino wa Hippo[3], tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu, hasa tarehe ya kifo chake[4].

Tazama pia

hariri

Maandishi yake

hariri

Tanbihi

hariri
  1. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/47550
  3. ""St. Sixtus III, Pope", Catholic News Agency, March 28, 2017". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-16. Iliwekwa mnamo 2022-04-10.
  4. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons

Lua error in package.lua at line 80: module 'Module:Navbar/configuration' not found.

  Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Sixtus III kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.