Pasiano (Hispania, 310 hivi - Barcelona, Hispania, 391 hivi) alikuwa askofu wa 2 wa mji huo kuanzia mwaka 365 hadi kifo chake.

Mt. Pasiano kadiri ya Joan Roig na Joan Moxí.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu na babu wa Kanisa[1].

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 9 Machi[2].

Maisha hariri

Aliwahi kuoa na kuzaa mtoto aliyefanya kazi ikulu.

Jeromu alisifu maisha yake matakatifu pamoja na usafi wa moyo, ujuzi na ufasaha[3].

Katika kuhubiri alikuwa akisema jina lake ni Mkristo na ubini wake ni Mkatoliki[4].

Maandishi hariri

Aliandika kuhusu mada mbalimbali, lakini vimetufikia kitabu kimoja juu ya toba na barua tatu tu[5].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.