Paulinus wa York

Paulinus wa York (alifariki 10 Oktoba 644) alikuwa mmisionari kutoka Roma nchini Uingereza aliyefanywa askofu wa kwanza wa York[1].

Saint Paulinus of York (cropped).jpg

MaishaEdit

Akiwa kati ya wamonaki waliotumwa na Papa Gregori I ili kuinjilisha Waangli na Wasaksoni, Paulinus alifika mwaka 604 katika kundi la pili.

Baada ya kuishi miaka huko Kent, tarehe 21 Julai 625 alipewa daraja takatifu ya uaskofu. Aliposindikiza Æthelburg wa Kent kwenda Northumbria kuolewa na Edwin wa Northumbria, alifaulu kumuongoa Edwin kuingia Ukristo pamoja na raia wake wengi. Kati yao alikuwepo Hilda wa Whitby. Pia alijenga makanisa kadhaa.

Edwin alipofariki (633), Paulinus na Æthelburg walikimbia Northumbria, wakimuacha nyuma James Shemasi. Huko Kent, Paulinus akawa askofu wa Rochester akapokea paliumu kutoka kwa Papa, ikiwa na maana ya kufanywa askofu mkuu wa York, ingawa hakupata nafasi ya kwenda[2].

Tangu kale Paulinus anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake.

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

 1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/92490
 2. Lapidge "Ecgbert" Blackwell Encyclopedia of Anglo-Saxon England

MarejeoEdit

   . http://www.oxforddnb.com/view/article/21626. Retrieved 6 March 2009.
   .
   .
   . https://archive.org/details/sim_english-historical-review_2002-09_117_473/page/889.

Marejeo mengineEdit

 • Mayr-Harting, H. M. R. E. (1967). "Paulinus of York". In G. J. Cuming. Studies in Church History IV: The Province of York. Leiden: Brill. pp. 15–21.
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.