Paliumu
Paliumu (kutoka Kilatini pallium) ni vazi linalotumika katika Kanisa la Kilatini.
Kwanza lilitumiwa na Papa wa Roma tu, lakini baadaye lilianza kutolewa naye kwa maaskofu wakuu kuonyesha mamlaka waliyonayo juu ya maaskofu kwa kushirikishwa na Ukulu mtakatifu.
Vazi lenyewe ni utepe mweupe uliotengenezwa kwa sufu ya mwanakondoo na uliotiwa misalaba myeusi sita: mine katika duara na miwili katika sehemu inayoangukia kifuani na mgongoni.
Utepe huo unavaliwa shingoni wakati wa adhimisho la Misa katika jimbo kuu na majimbo ya kanda yake, ila Papa anauvaa duniani kote kuonyesha hadhi yake kama mchungaji mkuu wa kundi lote la Kristo kadiri ya imani ya Kanisa Katoliki.
Maaskofu wa Ukristo wa Mashariki huwa wanavaa nguo inayofanana, lakini ni pana zaidi: omofori.
TanbihiEdit
MarejeoEdit
- Code of Canon Law regarding Metropolitan Archbishops, retrieved 2007-06-27
- Boniface (747), "Letter to Cuthbert, archbishop of Canterbury", translated by Talbot
- Canon 437, Code of Canon Law, 1983, IntraText library, retrieved January 29, 2015
- Kollmorgen, Gregor (25 January 2008), The Pallium - History and Present Use, New Liturgical Movement, retrieved 29 October 2014
- Paul VI (10 August 1978), "Motu Propio 'On The Conferring Of The Sacred Pallium'", L'Osservatore Romano (English weekly ed.): 3, archived from the original on 2017-01-06, retrieved 2017-10-10
- Rossa, Peter de (1988), Vicars of Christ: The Dark Side of the Papacy, Corgi, p. 137
- Skinner, Gerard (July 2011), The Pallium—a monograph published by the Archdiocese of Cardiff to mark the bestowal of the Pallium on Archbishop George Stack in July 2011.
- Schoenig, Steven A. (January 16–23, 2006), "The pope, the pallium, and the churches", America: 18–19
Viungo vya njeEdit
- A tradition in evolution: Pallium signifies authority, loyalty Archived 13 Mei 2006 at the Wayback Machine. (Catholic News Service)
- Information about the sisters, weaving the papal Pallium
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Paliumu kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |