Petro Fourier (Mirecourt, Lorraine, leo nchini Ufaransa, 30 Novemba 1565 - Gray, Burgundy, leo nchini Ufaransa, 9 Desemba 1640) alikuwa padri Mwaugustino aliyerekebisha jumuia za shirika lake na kuanzisha shirika la masista kwa ajili ya malezi ya bure kwa watoto fukara[1].

Sanamu ya rangi inayomuonyesha.

Akilazimika kwenda uhamishoni wakati wa Vita vya Miaka Thelathini, alijichagulia parokia fukara ya Mattaincourt akaishughulikia vizuri ajabu [2].

Papa Klementi XII alimtangaza mwenye heri tarehe 29 Januari 1730, halafu Papa Leo XIII alimtangaza mtakatifu tarehe 27 Mei 1897.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 9 Desemba[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  • Edward de Bazelaire, The life of the Blessed Peter Fourier, priest, reformer of a religious order and founder, London, Charles Dolman, 1850 (translated from the French) [1]
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.