Petro Nolasco

Petro Nolasco (kwa Kifaransa Pierre Nolasque; alizaliwa Mas-Saintes-Puelles, Ufaransa, 1189 hivi - Barcelona, leo nchini Hispania, 6 Mei 1256) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki anayekumbukwa hasa kwa juhudi zake za kukomboa Wakristo waliotekwa na Waislamu utumwani. Kwa ajili hiyo alianzisha utawa wa Wamersedari naye mwenyewe mwaka 1245 huko Algiers alijitoa kutekwa kwa niaba yao akapigwa hata karibu kufa.

Mtume Petro akimtokea Mt. Petro Nolasco; mchoro wa Francisco de Zurbarán, Museo del Prado, Madrid (Hispania.)

Anaheshimiwa kama mtakatifu hasa tarehe 6 Mei kila mwaka[1].

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

  1. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.