Posta ya Kijerumani Lamu

Posta ya Kijerumani katika mji wa Lamu, Kenya ni jengo la kihistoria na makumbusho ya kipindi cha ukoloni wa Kijerumani kwenye pwani ya Kenya.

Mfano wa sare ya wafanyakazi kwenye makumbusho ndani ya jengo la Posta ya Kijerumani mjini Lamu.

Jengo hili likasimikwa kama posta ya Dola la Ujerumani tarehe 22 Novemba 1888. Lamu haikuwa eneo la Kijerumani lakini ilikuwa bandari ya pekee iliyotembelewa na meli za Kizungu katika sehemu hii ya pwani. Zaidi ya hayo Lamu ilikuwa jirani na eneo la Usultani wa Witu ambayo iliwahi kuingia katika uhusiano wa ulinzi na Ujerumani tangu mwaka 1885.

Mradi wa kikoloni wa Kijerumani katika Witu ulianzishwa na Clement Denhardt na ndiye aliyeanzisha pia posta Kam kisiwani.

Posta hii ilifanya kazi kwa muda mfupi tu kwa sababu mwaka 1890 Ujerumani ilikabidhi eneo la Witu kwa Uingereza na ofisi ikafungwa tarehe 3 Machi 1891.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Posta ya Kijerumani Lamu kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.